29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Arusha kula sahani moja na watakaohujumu Anuani za makazi

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk. John Pima, amesema hawatamvumilia mtendaji au mtu atakayehujumu zoezi la anuani ya makazi.

Aidha, amewataka watendaji na wenyeviti wa mitaa kufanya zoezi hulo kwa uadilifu na kuzingatia taratibu walizowekewa katika mchakato huo.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Said Mtanda.

Akizungumza juzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wenyeviti na watendaji wa mitaa yote katika halmshauri hiyo,amessma watendaji hao wanapaswa kufanya zoezi hilo kwa uadilifu na kulipa kipaumbele.

“Hili ni zoezi nyeti na maalum la kitaifa,zingatieni utaratibu na mjitume mfanye kazi kwa weledi kwani hatutavumilia mtu atakayetuhujumu,” amesema Pima.

Mkurugenzi huyo amesema kata ambazo wataanza nazo ni Kaloleni,Kati,Levolosi,Themi na Sekei na kuwa kuanzia Februari 15,2022 baadhi ya kazi zitaanza kufanyika ambapo watendaji na wenyeviti wa mitaa ndiyo wataitiaga vikao na kuanza utambuzi wa barabara kwenye maeneo yao.

Awali, akizungumza na vijana walioteuliwa kwenye zoezi la kubandika anuani za makazi katika kata hizo,amewataka kufanya kazi hiyo kwa makini na weledi.

Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya hiyo,Said Mtanda,amewataka watendaji na wneyeviti hao kutoa elimu ya umuhimu wa zoezi hilo katika maeneo yao ili kuepuka maneno ya uvumi yenye nia ya kuvuruga zoezi hilo.

Amesema wananchi wasipoelewa vizuri zoezi hilo wakitokea watu wneye fitina watapotosha jamii.

“Zoezi hili ni zuri kwa kuwa mnashirikisha wadau wote ikiwemo viongozi wa dini hivyo mkafanye kazi kwa mshikamano na kutoa elimu kwa wananchi,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles