27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NACTVET yazuia wanafunzi 2,854 kujiunga na vyuo kutokana na kukosa sifa

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limesema limezuia wanafunzi 2,854 kutokana na kukosa sifa ya kusoma Programu mbalimbali katika Vyuo vya kati na vya ufundi nchini katika mwaka wa masomo 2020/2021.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Februari 16, na Katibu Mtendaji wa Baraza la hilo, Dk. Adolf Rutayuga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma baada ya ufunguzi wa kikao cha siku mbili na Wawakilishi wa Vyuo vya kati na ufundi na Maafisa wanaoshughulikia udahili katika vyuo hivyo nchini.

Katibu Mtendaji huyo amesema wao kama Baraza wamekuwa na udhibiti wa udahili kwa vyuo ambavyo vimekuwa vikiwadanganya wanafunzi ambapo amedai sifa za mwanafunzi kuweza kudahiliwa ni kuwa na D nne.

“Kuna wanafunzi 2,854 ambao waligundulika kwamba hawakuwa na sifa ya kusoma Programu mbalimbali ambazo Vyuo vya kati na ufundi vilikuwa vimewasilisha majina yao.

“Kama Baraza tusingekuwa na udhibiti wa udahili inamaana hawa wanafunzi walikuwa wanapotezewa muda wao kwa hiyo tulivitaarifu vyuo na ukaambiwa mmewadanganya ambapo muongozo wa udahili unaeleza lazima wawe na sifa gani,” amesema Dk. Rutayuga.
Amesema lengo la kikao hicho ni kujadiliana changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza katika masuala ya udahili nchini.

“Tunautaratibu wa kukaa na wadau wetu kuhusiana na udahili na  changamoto zipi zimepatikana ili kuweza kuzitatua kwa sababu ya wingi wa vyuo tutakutana nao kwa siku mbili hapa,” amesema.

Amesema changamoto kubwa ambayo wanaiona ni iwapo miongozo ya udahili haitafuatwa hutokea  matatizo makubwa kwa wanafunzi kwani hutumia muda mrefu kuwa chuoni huku wakiwa  hawana  sifa.

“Kikubwa ambacho tunakiona ni kama miongozo ya udahili haitafuatwa ni matatizo makubwa sana tutawasababishia wadau wetu ambao ni wanafunzi wanaosoma Programu hizo pamoja na wazazi wao na jamaa zao wanaowalipia ada kwa kusoma vyuo ambavyop havijasajiliwa.

“Vyuo vinavyofanya hivyo havifanyi jambo zuri mwingine anasoma miaka mitatu halafu anaambiwa hatambuliki. Tunamiongozo ya udahili ambayo inaeleza kila chuo kimesajiliwa kwa namba fulani na kinatakiwa kutoa mikopo na sifa za kuingia katika program hiyo.
“Kila program inasifa zake za kuingilia na angalau uwe unaufaulu wa  alama D nne na zinaeleza kwenye masomo yapi,” amesema Dk. Rutayuga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles