29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatenga bilioni 1 MAKISATU

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetenga Sh bilioni 1 kwa ajili ya kuendeleza wabunifu watakao tambuliwa katika mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu(MAKISATU) mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo, Februari 16, jijini Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya wiki ya MAKISATU kwa mwaka 2022.

Prof. Mkenda amesema maadhimisho ya wiki ya MAKISATU yanalenga kuibua, kutambua na kuendeleza jitihada zinanzofanywa na wabunifu wa kitanzania na kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Amesema wiki ya ubunifu ni sehemu ya mikakati ya serikali ya awamu ya sita ya kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo za kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii.

Prof. Mkenda amesema wiki ya ubunifu inaandaliwa kwa kushirikiana na program ya FUNGUO ya UNDP na itafanyika katika mikoa 17 nchini.

Mikoa shiriki ni Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Arusha, Iringa, Mwanza, Zanzibar, Tanga, Kilimanjaro, Morogoro, Njombe, Kagera, Mtwara, Kigoma, Mara na Ruvuma.

Amesema   wiki hiyo ya kitaifa ya ubunifu kwa mwaka 2022 itaadhimishwa kuanzia Mei 15 hadi Mei 20 mwaka huu katika jiji la Dodoma itakayoenda sambamba na kilele cha MAKISATU.

“Usajili wa ubunifu kwa ajili ya Mashindano ulifikia mwisho tarehe 10, Februari, 2022, Lakini kutoka na uhitaji, Leo nichukue fursa hii kutangaza rasmi, kuongeza muda wa usajili wa Wabunifu hadi Februari 28 mwaka huu na hadi kufikia jana tarehe 15 Februari, tumesajili wabunifu zaidi ya 480 kwa ajili ya Mashindano,” amesema Waziri Mkenda.

Pia amesema kuwa mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, washiriki watatoka katika makundi saba ambayo ni Shule za Msingi Shule za Sekondari Vyuo vya Ufundi Stadi Vyuo vya Ufundi Vyuo Vikuu Taasisi za Utafiti na Maendeleo na Mfumo usio Rasmi.

Amesema usajili wa washiriki wa MAKISATU mwaka huu ulianza rasmi tangu Desemba 27 mwaka 2021 na usajili huo unaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikishirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inayosajili wabunifu wa makundi ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Utafiti na Maendeleo.

“Katika kilele hicho kutakuwa na maonesho ya teknolojia na bunifu mbalimbali, bidhaa na huduma zinazotolewa na taasisi zitakazoshiriki zikiwemo taasisi za kitafiti na maendeleo, Vyuo Vikuu, kumbi za ubunifu, taasisi za kibiashara, wakala za Serikali, Wizara na Taasisi binafsi na pia katika kilele hicho kutakuwa na utoaji tuzo kwa wabunifu 21 walioshinda MAKISATU,”amesema.

Prof Mkenda amesema  kupitia MAKISATU 2019, 2020 na 2021, Wizara imefanikiwa kuibua na kutambua wabunifu wachanga 1,785.

Amesema kupitia wabunifu hao bunifu 466 zilikidhi vigezo, zimetambuliwa na kuhakikiwa na kati ya hizo bunifu mahiri 200 tayari zinaendelezwa na Serikali ili kufikia hatua ya kubiasharishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles