26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

MKULIMA MWINGINE AJERUHIWA KWA SIME KILOSA

524332cd04985aff0de9f1e645398d62

Na RAMADHAN LIBENANGA- KILOSA

MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Mamoyo, Kata ya Mabwerebwere, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Omary Sululu (52), amenusurika kifo baada ya kukatwakatwa na sime kichwani na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji.

Taarifa zilizopatikana kijijini hapo, zinasema Sululu alijeruhiwa na wafugaji hao wakati alipokuwa akizuia mifugo isile mazao katika shamba lake.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Joshua Lugaso, kutoa tamko la  kulaani matukio ya kikatili yanayofanywa  na  wafugaji dhidi ya wakulima wilayani Kilosa.

Akizungumza na MTANZANIA akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa, Sululu alisema alijeruhiwa Januari mosi, saa za mchana wakati alipokuwa katika shamba lake la mahindi na migomba.

“Nilipokuwa shambani, niliona kundi la ng’ombe likiingia shambani kwangu na nilipokuwa katika harakati za kuwafukuza mifugo hao, wafugaji watatu walitokea kichakani wakiwa na marungu, sime na fimbo.

“Waliponikaribia, walinitaka niiache mifugo iendelee kula mazao yangu kwa sababu ilikuwa na njaa. Wakati nikijibizana nao, mifugo hiyo ilikuwa inaendelea kula mazao yangu.

“Baadaye walijitokeza wafugaji wanane wakiwa na silaha mbalimbali na kunihoji kwanini ninazuia mifugo isile chakula.

“Kisha walinizunguka wakaanza kunipiga na marungu kichwani, walinikata na sime kichwani na kuniangusha wakati nimepoteza fahamu.

“Walipoona nimeanguka chini, walikimbia na mifugo yao, lakini baada ya kama dakika 15 hivi alitokea dereva wa pikipiki ambaye aliniinua na kunipeleka hadi kituo cha polisi,” alisema Sululu.

Kaimu Mganga Msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa, Thomas Kibula, alithibitisha kumpokea Sululu hospitalini hapo akiwa na majeraha kichwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles