26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mkakati wa Malinyi kujinasua kutoka mkiani

Mbunge wa Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro, Dk. Hadji MpondaNa Mwandishi Wetu, Malinyi

WILAYA ya Malinyi iliyoko mkoani Morogoro ni miongoni mwa wilaya mpya iliyogawanywa kutoka Wilaya ya Ulanga.

Miongoni mwa shule za sekondari zilizoko wilayani humo ni Malinyi, Igawa na Sofi ambazo ni zimekuwa za mwisho katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015.

Shule zingine za mwisho katika matokeo hayo ni Pande (Lindi), Korona (Arusha), Kurui ya (Pwani), Patema (Tanga), Saviak (Dar es Salaam), Gubali (Dodoma) na Kichangani (Morogoro).

Kufuatia shule hizo kufanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne, sekta ya elimu wilayani humo imeamua kuweka mkakati wa kuinua kiwango cha taaluma ili kuepukana na aibu iliyoipata mwaka 2015.

Ofisa Elimu Taaluma wa Wilaya ya Malinyi, James Nicodem, anasema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi licha ya serikali kuweka mkakati wa kupeleka walimu katika kila wilaya kila mwaka.

Anasema kufuatia upungufu huo wamejipanga kugawa walimu kwa kuzingatia uhitaji wa walimu kwa kila shule ili kuondoa au kupunguza uhaba huo mara baada ya kupokea walimu kutoka serikalini.

“Tunafikiria kupeleka walimu katika shule ambazo hazina kabisa, ikiwemo Shule ya Sekondari Kipingu yenye wanafunzi 704 huku ikiwa na mwalimu mmoja tu wa somo la fizikia anayefundisha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne,” anasema Nicodem.

Kulingana na ofisa huyo, wilaya inakabiliwa na upungufu wa walimu 145.

Naye Mwalimu wa Shule ya Sekondari Malinyi, Anslem Mponji, anasema shule hiyo ilikuwa na watahiniwa 56 na kati yao 40

Walipata daraja sifuri, 12 daraja la nne na wengine wanne matokeo yao yakizuiliwa.

anaiomba Serikali kuhakikisha inajenga nyumba za walimu karibu na maeneo ya shule jambo litakalofanya wanafunzi wanaotoka umbali mrefu kubaki shuleni wakifundishwa masomo ya ziada na walimu wao.

“Wazazi nao wabadili mtazamo na kuamka katika suala zima la elimu kwa sababu katika wilaya yetu hii wazazi wengi huamini kuwa mtoto anaweza kufanikiwa akizingatia sana kilimo na si elimu,” anasema Mponji.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Malinyi, Dk. Khadji Mponda,   anasema wameshaanza kuweka mikakati ya kunusuru suala la elimu wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wazazi wanashirikiana na walimu kukagua kazi za wanafunzi.

“Nimesikitishwa sana na taarifa za kufeli kwa wanafunzi kwenye shule tatu wilayani humu tutahakikisha tunaendelea kutoa chakula kwa wanafunzi ili kuongeza ari ya kusoma,” anasema Dk. Mponda.

Pia anaiomba Serikali kuharakisha kupeleka walimu wa masomo ya sayansi ili kukidhi mahitaji ya shule zote za wilayani humo.

Kulingana na mbunge huyo, wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya mfumo mbovu wa usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza hali inayochangia kuwapo kwa matokeo mabaya hasa katika mitihani ya kitaifa.

“Kuna matatizo ambayo yamekuwa yakijirudia karibu kila mwaka, utakuta wanasajili wanafunzi wa kidato cha kwanza wasiojua kusoma wala kuandika, sasa kwa hali hii tutegemee matokeo yatakuwa mazuri,”? anahoji.

Mbunge huyo anasema pia uchanga wa wilaya pia unachangia kiwango cha elimu kushuka kufuatia walimu kutokuwa na moyo wa kwenda kufanya kazi wilayani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles