23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mjadala mzito wa bajeti kuanza leo

Na ANDREW MSECHU

-DAR ES SALAAM

MJADALA mzito wa mapendekezo ya bajeti kuu ya Serikali mwaka 2019/20, unaanza leo jijini Dodoma ambapo wabunge wanatarajia kuipitia, kisha kuipitisha.

Mapendekezo hayo ya bajeti yaliwasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wiki iliyopita.

Katika mjadala huo wa siku tano, Serikali inaliomba Bunge kuidhinisha Sh trilioni 33.1, kwa matumizi yake kwa mwaka wa fedha unaotarajiwa kuanza Julai mosi. 

Wakati wabunge wakitarajiwa kuanza mjadala huo, jana kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema ni vyema Serikali iangalie uwezekano wa kupunguza makato yatokanayo na mishahara ya wafanyakazi (PAYE) ili kuwapa ahueni.

Zitto alisema ipo haja ya kuangalia upya na kupunguza viwango vya makato hayo.

Alisema chama chake kinapendekeza kuondolewa kabisa kwa makato kwa mshahara au mapato ya jumla ya kila mwezi yasiyozidi Sh 360,000.

“Tunapendekeza makato yanayoanzia Sh 360,000, lakini yanayozidi kiwango hicho, ndiyo yaanze kukatwa asilimia 11 ya VAT, yaendelee kwa viwango tofauti hadi asilimia 40 kwa mapato yanayozidi Sh milioni 15,” alisema.

Alisema ACT-Wazalendo pia inapendekeza kushuka kwa makato ya wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii hadi asilimia 12, kutoka asilimia 20, yaani 10 kwa mwajiriwa na 10 kwa mwajiri kama ilivyo kwenye sheria ya baadhi ya mifuko kwa sasa.

“Hapa kwenye asilimia hii, mwajiri atakuwa na asilimia yake na mwajiriwa atakuwa na asilimia yake, kuna nchi jirani kama Kenya wanatumia asilimia tisa ya makato na wanafanya vizuri,” alisema.

Akizungumzia uamuzi wa Serikali kurudisha kodi kwenye taulo za kike, alisema ingeweza kuepukwa kwa kuangalia namna ya kusaidia zaidi akina mama.

Hata hivyo, wakati akiwasilisha bajeti hiyo, Dk. Mpango alisema Serikali imefuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) uliokuwa unatolewa kwenye taulo za kike kwa kuwa haujawezesha kupatikana kwa bidhaa hiyo muhimu kwa bei nafuu kwa walengwa na badala yake unawanufaisha wafanyabiashara. 

“Wakati Serikali ilipoweka msamaha huu, ilitarajia wazalishaji wa taulo za kike wataziuza kwa bei nafuu baada ya kusamehewa kodi,” alisema Dk. Mpango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles