27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Miundombinu bora yatajwa kivutio cha uwekezaji

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert Chalamila, amesema Serikali baada ya kuweka mazingira bora ya uwekezaji kuboresha sera, miundombinu imeendelea kuvutia wawekezaji nchini

Akizungumza leo Desemba 16,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni ya Derm Group.

“Miaka 25 si mchezo, niwapongeze sana uongozi na wafanyakazi wote wa Derm Group kwa kuadhimisha miaka 25 tangu mlipoanza shughuli zenu hapa nchini.

“Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, siku zote imekuwa bega kwa bega na sekta binafsi ambazo zimekuwa zikishirika kwa namna moja ama nyingine katika ujezi wa Taifa letu kwa kutoa ajira kwa Watanzania na ushalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali,” amesema Chalamila.

Amesema serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wowote watakaohitaji ili kuendeleza gurudumu la maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Ridhuan Mringo amesema wanajishughulisha na mambo ya ujenzi, huku ikijivunia mfanikio makubwa waliyoyapata katika shughuli yao hiyo.

“Mafanikio haya hayajaja hivi hivi, bali yametokana na mipango na mikakati thabiti ya uongozi kwa kushirikiana na wafanyakazi wetu wote ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa,” amesema Maringo.

Amesema kuwa pia Serikali za awamu zote tangu walipoanza shughuli zao, zimekuwa zikiwapa ushirikiano mkubwa, jambo ambalo limechangia kwa kukua.

“Nitoe pongezi za dhati kabisa kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk, Samia kwa jinsi ilivyochangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa kampuni yetu ndani ya miaka hii michache tangu Mama yetu aliposhika madaraka.

“Kwa kweli tumepiga hatua kubwa sana kutokana na jinsi Serikali ilivyotujengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zetu hapa nchini bila wasi wasi wowote,” amesema Mringo.

Amesema kuwa kampuni yao iliyoanza mwaka 1998, imefanikiwa kutoa ajira ya kudumu kwa zaidi ya Watanzania 500, wakiwa ni wanaume na wanawake, wanaohusika katika nyanja zote za shughuli zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles