23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk.Ashatu: Tuna sababu  kuwalinda wawekezaji

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk.Ashatu Kijaji  amesema wana sababu ya  kuwalinda wawekezaji  wenye viwanda nchini kutokana na kutoa ajira kwa wananchi.

Dk. Ashatu amebainisha  hayo leo Desemba 21,2023 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea  kiwanda cha Chemicotex kilichopo Mbezi Beach Jogoo  kwa lengo la  kuona bidhaa wanazozalisha na kuongea na wafanyakazi.

Amewaomba  vijana wa kitanzania kuwa  waadilifu na kujituma wanapopata ajira kwa kuweka  kipaombele kwenye kufanya kazi  ambazo wameaminiwa ili waendelee kunufaika kwa pamoja na kuimarisha uchumi wao na Taifa.

“Nimpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa sababu ametengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na ufanyaji biashara,tunaona wawekezaji wanafuraha na amani wamekuja kuwekeza na wanaendelea  kuzalisha,”amesema Dk. Ashatu.

Amesema kiwanda hicho cha mzawa kimeajiri  watanzania 1000wanafanyakazi kiwandani na zaidi ya 1000  wanauza  nje bidhaa.

Amesema kwa sababu  kila unapokwenda unakutana na bidhaa  za kiwanda hicho,ni muhimu kutambua kuwa  wanatengeneza  ajira  kwa vijana  na wanapata faida hivyo mitaji yao ipo salama.

Ameeleza kuwa kilichompa faraja zaidi  asilimia 60 ya wafanyakazi  1000 ni wanawake.

“Sisi tupo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  mmesikia bidhaa inayotengeneza hapa inauzwa kwenye nchi sita ndani ya Afrika na duniani tunapeleka bidhaa zetu,”ameongeza.

Aidha amesema wanaendelea kuimarisha Tanzania ya viwanda wanapotekeleza katika  Dira ya Taifa wanakwenda kuhitimisha mwaka 2025 na kusisitiza viwanda ndio sehemu pekee watanzania wengi wanapata ajira.

Amesema wanavyojua dunia  ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda, hata dira inayoandaliwa sasa itawapa nafasi kubwa wenye viwanda.

Aidha  ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda kuendelea kufurahia mazingira bora ya ufanyaji biashara.

Naye Mwenyekiti wa Kiwanda cha Chemicotex, Yogesh Manek amesema leo wamepata bahati  ya kutembelewa na Waziri  na kuona bidhaa wanazozalisha.

Amesema katika kiwanda hicho wanazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo dawa za meno vipodozi na zinginezo.

“Asilimia kubwa ya watanzania wanatumia bidhaa ya kiwanda hiki tumeajiri jumla ya watu 1000 kati ya hao 550 wanawake na 450 wanaume na walemavu sita hii  ni fursa kwa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi,”amesema Manek.

Aidha amesema hali ya biashara kwa sasa ni nzuri kwa sababu wana fursa ya kufanya kazi na wanapeleka bidhaa zao nchi sita ikiwemo Rwanda, Unganda Uganda, Kenya, Burundi na Congo pamoja na soko la Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles