27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mitihani kidato cha sita yaanza

shukuru-kawambwaGrace Shitundu na Michael Sarungi, Dar es Salaam
MTIHANI wa kidato cha Sita ulioanza jana nchini kote umeendelea licha ya mgomo wa madereva uliofanyika na kusababisha tatizo la usafiri.
Mtanzania ilifanikiwa kuzunguka katika baadhi ya shule zilizopo katikati ya jiji la Dar es Salaam ambazo ni Tambaza, Jangwani na Azania na kukuta wanafunzi wakiendeleea na mitihani yao.
Hata hivyo baadhi ya walimu waliliambia gazeti hili kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wamechelewa kufika katika chumba cha mtihani kutokana na tatizo la usafiri.
“Wakati nikiwa katika kituo cha daladala eneo la Ubungo niliona wanafunzi wawili wa shuleni kwetu wakitembea kwa miguu ili wakafanye mtihani, ilibidi niwakodishie bajaji ili wawahi mitihani yao,” alisema mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Azania.
Akizungumza na gazeti hili Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa, alisema mgomo wa vyombo vya usafiri unaoendelea haujaathiri kwa namna yoyote mitihani hiyo.
Alisema alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule na hakuna taarifa zozote za mwanafunzi kushindwa kufanya mitihani kutokana na mgomo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles