27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mkulima aliwa na simba shambani kwake

NA AMINA OMARI, MKINGA
MKULIMA mmoja mkazi wa Kijiji cha Mlima kilichopo Kata ya Mwakijembe, wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, Silyvester Msubari, amefariki dunia baada ya kuliwa na simba.
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza, alisema jana kuwa mkulima huyo aliuawa juzi alfajiri wakati alipokuwa shambani kwake akilinda mazao yake yasiharibiwe na wanyama.
“Siku ya tukio, marehemu alikuwa shambani kwake akilinda mazao yake yasiharibiwe na wanyama.
“Wanyama hao wamekuwa wakizagaa mashambani kwa sababu Kata ya Mwakijembe inapakana na Hifadhi ya Mkomazi yenye wanyama mbalimbali.
“Kwa hiyo nawaomba wananchi wawe na tahadhari muda wote pindi wanapokwenda mashambani kulinda mazao yao ili wanyama wakali wasiwadhuru.
“Ikibidi wananchi wawe katika makundi ili wanyama wakali wakiwavamia iwe rahisi kwao kukabiliana nao vinginevyo watazidi kupoteza maisha,” alisema Mgaza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles