26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mitandao ya Kijamii itumike vizuri

Na John Morice Obadia

Ndugu Mhariri, katika zama hizi za mitandao ya kijamiii tumeona mambo mengi, mengine wala hatukuwahi kufikiri tutayaona.

Kuna wengine wanatumia vizuri hii mitandao kwa biashara, kuwasiliana na ndugu na jamaa au hata kujifunza.

Changamoto ni pale mitandao hii inapotumika vibaya na kusababisha msongo wa mawazo, uhalifu, chuki au hata kuchochea uadui kati ya pande mbili. Hayo yote tunayaweka katika kundi la matatizo ya afya ya akili.

Kujilinganisha na watu na kujiona masikini, mbaya wa maumbile au mtu aliyechelewa kwenye maisha kunaleta msongo wa mawazo na wengine mpaka wanashawishika kuiba mali wapige nazo picha wajione na wao wapo vizuri kifedha.

Tunaona namna baadhi ya wasanii na watu maarufu wanavyo gombana mitandaoni na kufanya watu wawatukane na kuwadhalilisha.

Niwashauri Watanzania wenzangu tujifunze kutumia mitando kujijenga kiakili, kimwili, kiroho hata kiuchumi.

Tukicheza na afya ya akili hata kazi zetu za kila siku tutashindwa kutoa matokeo chanya na tutavunja mahusiano na watu wetu wa karibu.

Mwandishi wa barua hii ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles