28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Mista Champagne aliwinda penzi la Gigy Money

Bujumbura, Burundi

Staa wa muziki na vichekesho nchini Burundi, Mista Champagne, ameonyesha nia ya kulitaka penzi la mrembo wa Tanzania, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kwa gharama yoyote.

Mista Champagne

Mista Champagne, ambaye hivi karibuni ameachia albamu yake, Niatari Kweli, amekuwa na kawaida ya kumchombeza Gigy Money kwenye mtandao wa Instagram huku akimtambia kwa fedha nyingi alizonazo kiasi cha kupachikwa a.k.a ya Ginimbi wa Burundi.

Harakati za Mista Champagne kumnasa Gigy Money zilionesha kuzaa matunda hivi karibuni baada ya mrembo huyo kutaka uthibitisho kutoka kwa Champagne kama kweli ana fedha za kutosha ili aweze kuruka naye.

Aidha Champagne anatarajia kutua Tanzania hivi karibuni kwaajili ya kutangaza albamu yake (Niatari Kweli) pamoja na kujaribu bahati yake ya kumnasa Gigy Money.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles