NA THERESIA GASPER,
WAREMBO wanaoshiriki mashindano ya Miss Sinza juzi walianza kambi rasmi katika Hoteli ya Den France, Dar es Salaam, kujiandaa na shindano linalotarajiwa kufanyika Julai 29 mwaka huu.
Akizungumza na MTANZANIA jana, mratibu wa mashindano hayo, Nasib Mahinya, alisema mshindi atayepatikana atapata fursa ya kushiriki Miss Kindondoni na baadaye kwenda Miss Tanzania.
“Tumeanza mazoezi ili kuwaandaa kuwa fiti huku tukiwa bado tunaendelea kuwapokea washiriki wengine wanaohitaji kwa sababu nafasi bado zipo,” alisema.
Baadhi ya wadhamini wa mashindano hayo ni New Habari Limited, Mabibo Bia, Hoteli ya Den France, Clouds Media na Big Solution.