27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Minoti ya zawadi yamchanganya Pastor Myamba

Mwigizaji wa filamu nchini, Emmanuel Myamba
Mwigizaji wa filamu nchini, Emmanuel Myamba

NA PAULINA LYAPA (TUDARCO)

MWIGIZAJI wa filamu za bongo, Emmanuel Myamba, maarufu kwa jina la Pastor Myamba, amesema hakutegemea kupata kiasi kikubwa cha zawadi ya fedha katika sherehe ya harusi yake iliyofanyika Visiwani Zanzibar katika ukumbi wa Bwawani, hali ambayo anaona inamchanganya.

Katika sherehe hiyo, mwigizaji huyo alipokea zawadi mbalimbali kutoka ndugu, jamaa na marafiki wa karibu, zikiwemo fedha alizokabidhiwa na kamati zilizobebwa kwenye kitoroli kama mzigo, gari na vitu vingine mbalimbali.

Akizungumza na MTANZANIA, Pastor Myamba alisema hakutarajia kupata zawadi kubwa kama alizopata, alijua kutakuwa na zawadi lakini si kama alivyoziona.

Alisema anamshukuru Mungu mipango yake ya ndoa imekwenda vizuri.

“Namshukuru Mungu kwani sikutarajia kilichotokea, watu walijitoa kwa wingi, namshukuru dada yangu ambaye ndio kama mama aliyenilea kwa zawadi ya gari pamoja na kamati iliyonizawadia pesa ambazo mpaka sasa siwezi kusema ni shilingi ngapi,” alisema.

Alisema kila jambo linapangwa na Mungu, hivyo hana budi kumshukuru kwa zawadi ya maisha na furaha aliyojaaliwa pamoja na wote waliokuwa kwenye upande wake katika harusi hiyo.

Myamba ameingia katika chama cha wanandoa na kuzawadiwa mamilioni ya pesa kutoka kwa kamati ya maandalizi pamoja na gari alilopewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles