28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mikoa ya Shinyanga, Singida kinara uharibifu wa mazingira

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

MIKOA ya Shinyanga, Singida na mingine yenye asili ya kame na Tabia ya nchi imetajwa kuwa kinara wa uharibifu mkubwa wa mazingira ni.

Akizungumza leo Aprili 27, 2023 jijini Dar es Salaam katika mkutano ulio wakutanisha wadau mbalimbali wa misitu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI), Dk. Revocates Mushumbusi amesema lengo ni kujadili uokoaji wa asili.

“Uharibifu wamazingira ni mkubwa sana unaotokana na matumizi ya binadamu ikiwemo kilimo cha kuhamahama, ufugaji, vyanzo vya maji na kushindwa kufuata utaratibu wa mipango miji,” amesema Dk. Mushumbusi.

Amesema katika nchi 32 za Afrika zilizokaa mwaka 2018 lengo ni kureejesha hekta milioni mia moja za uoto wa asili ifakapo 2030.

“Ni utekelezaji wa mkakati wa nchi za Afrika Tanzania ni miongoni nchi zitarejesha hekta milioni tano nza uoto wa asili ifikapo mwaka 2030,” amesema Dk. Mushumbusi.

Aidha, amesema ahadi kubwa waliyonayo ni kuendelea kutoa elimu jinsi ya kurejesha uoto wa asili.

Naye, Mhifadhi Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu, Juma Mwangi amesema
Hekta 469,000 huaribiwa kwa mwaka kutokana na kuanzisha makazi mapya na mengineyo.

“Mkutano huo utafungua fursa mbalimbali kwa wadau na kusaidia uongoaji wa ardhi iliyoharibika na kuhakikisha ardhi inarudi kama ilivyokuwa,” amesema Mwangi.

Naye Mkurugenzi wa Miradi Kisiki Hai, Njamasi Chiwanga amesema Taasisi yao lengo ni kukusanya nguvu ili kutimiza malengo hayo.

“Taasisi yetu zaidi ya asilimia 55 tunafanya kazi hivyo zaidi ya Vijiji mia nne misitu iko chini yao tuna mikakati mingi ya kurejesha ardhi na uoto wa asili,” amesema Chiwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles