26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Miezi 13, makocha 3 Simba

aveva

 

NA  ABDUCADO EMMANUEL,
DAR ES SALAAM

INASHANGAZA! Hiyo ndio hali halisi kwa timu ya Simba baada ya kunolewa na makocha watatu tofauti ndani ya miezi 13 iliyopita hadi sasa. Simba tayari imemfuta kazi kocha wake Mzambia, Patrick Phiri, aliyeanza kuinoa timu hiyo Agosti mwaka jana na nafasi yake imechukuliwa na Mserbia, Goran Kopunovic, aliyetarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja jana.
Goran anakuwa kocha wa tatu kuinoa Simba ndani ya miezi 13 iliyopita kwani kabla ya Phiri kurejea, kibarua cha kocha mwingine wa timu hiyo raia wa Croatia, Zdravko Logarusic kiliota nyasi. Loga aliyeanza kazi Simba Desemba 1, mwaka juzi alipewa mkataba mpya wa mwaka mmoja Julai, mwaka jana na alitimuliwa mwanzoni mwa mwezi Agosti baada ya kufungwa mabao 3-0 kwenye mechi ya ‘Simba Day’ dhidi ya Zesco United ya Zambia.
Uongozi wa Simba kupitiakwa Rais wake, Evans Aveva, ulidai kuwa umemtimua Loga baada ya kuchoshwa na tabia zake zinazojirudia, lakini taarifa zingine zilidai walikosa imani naye hasa baada ya timu hiyo kucheza vibaya dhidi ya Zesco. Mbali na hilo, pia Simba imetimiza idadi ya makocha wanne kuanzia msimu uliopita hadi sasa ligi ikiwa bado haijamaliza mzunguko wa
kwanza.
Ukiachana na makocha hao watatu, kocha mwingine wane aliyeinoa ni mzawa, Abdallah Kibadeni aliyekuwa akisaidiana na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, waliotimuliwa baada ya kumalizika mzunguko wa kwanza wa msimu uliopita na nafasi zao kuchukuliwa na Loga na Selemani Matola.
Phiri anaondoka akiwa ameiacha Simba katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), ikiwa na pointi tisa baada ya kuambulia sare sita, ushindi mechi moja na kufungwa mchezo mmoja. Goran alitarajiwa kuishuhudia kwa mara ya kwanza timu hiyo jana usiku wakati ikicheza na Mtibwa Sugar kwenye mechi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi lililoanza jana, Visiwani Zanzibar.
Mserbia huyo aliwahi kuinoa timu ya Police ya Rwanda kwa misimu mitatu na kufanikiwa
kuijengea heshima timu hiyo na kushindana na vigogo wa nchi hiyo Rayon Sports na APR.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles