KULWA MZEE, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Mhasibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sereki Mesack amedai mahakamani kuwa haoni kama kuna tatizo katika stakabadhi zenye thamani ya Sh milioni 25 na Dola za Marekani 27,500 ambazo aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo, Jamali Malinzi alilikopesha shirikisho hilo.
Shahidi huyo wa tisa wa upande wa Jamhuri amesema hayo leo Decema 5 saa tano asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wakati alipokuwa akitoa ushahidi.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Mwandamizi Shadrack Kimaro, shahidi huyo amesema kazi yake ilikuwa ni kuingiza stakabadhi na nyaraka za malipo katika kompyuta na fedha ambazo Malinzi aliikopesha TFF zilikuwa kwa ajili ya kuiwezesha timu ya mpira wa miguu ya vijana chini ya miaka 17 kwenda nchini Afrika Kusini, Rwanda na Kongo.
Shahidi huyo ameongeza kuwa fedha zingine alikuwa anaikopesha TFF na aliongeza kwamba tuhuma kuwa aliliibia shikirikisho hilo kasikia Takukuru baada ya kumshtaki Malinzi na wenzake wanne.
Malinzi anawakilishwa na Wakili, Richard Rweyongeza aliyetaka kufahamu kama aliyeulizwa anafahamu kuwa Malinzi anadaiwa kuiba fedhaambapo shahidi alijiu kuwa alizisikia tuhuma hizo baada ya kushtakiwa.