33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MHARIRI BBC AJIUZULU

BEIJING, CHINA


MHARIRI wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini China, Carrie Gracie amejiuzulu kwa sababu ya kutoridhishwa na usawa wa mshahara na wafanyakazi wenzake wa kiume.

Kwenye barua yake, Gracie ambaye amefanya kazi na BBC kwa zaidi ya miaka 30, amemlaumu mwajiri wake kwa ubaguzi katika malipo.

Alisema BBC inakumbwa na tatizo la kuaminiwa baada kufichuliwa kwa taarufa kuwa theluthi mbili ya wanahabari maarufu wanaolipwa zaidi ya pauni 150,000 ni wanaume.

Lakini BBC imejitetea kuwa hakuna ubaguzi dhidi ya wanawake katika mpango wake wa ulipaji mishahara.

Gracie alisema amejiondoa katika wadhifa wake wa uhariri wa ofisi ya BBC mjini Beijing wiki iliyopita lakini atabakia kufanya kazi BBC.

Alisema atarudi kwa wadhifa wake wa zamani katika chumba cha habari cha televisheni ambako anatarajiwa kulipwa sawa na wengine.

Julai mwaka jana, BBC ililazimika kufichua mishahara ya wafanyakazi wote wanaolipiwa zaidi ya pauni 150,000 kwa mwaka.

Gracie alisema alishangaa kugundua kuwa wahariri wawili wa kiume wa kimataifa wa BBC, walilipwa asilimia 50 zaidi kuliko wenzao wawili wa kike.

Mhariri wa Marekani, Jon Sopel analipwa kati ya pauni 200,000 hadi 249,999 huku mhariri wa Mashariki ya Kati, Jeremy Bowen akilipwa kati ya pauni 150,000 hadi 199,999.

Gracie hakuwa katika orodha hiyo ikimaanisha kuwa mshahara wake ulikuwa chini ya pauni 150,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles