Safina Sarwatt, Moshi
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameupongeza Uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Moshi Mjini (MUWSA), kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya maji taka.
Pongezi hizo amezitoa leo Desemba 13, wakati wa ziara yake ya kwanza ya kikazi mkoani Kilimanjaro, tangu ateuliwe kushika wadhfa huo, alipotembelea eneo la mabwawa ya kutibu maji taka yaliyopo Kata ya mabongini mkoani humo, kwa lengo la kujionea shughuli za ukarabati wa mabwawa hayo.
Mhandisi Mahundi amesema huduma za maji taka hapa nchini haiko vizuri na hivyo kuzitaka Mamlaka za maji kote nchini kuhakikisha kwamba wanachi wake wanaunganishwa kwenye mifumo ya maji taka.
Kwa upande wak, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA), Mhandisi Kija Limbe, amesema mabwawa ya maji taka kwa sasa yamezidiwa kutokana na uwezo wake kuwa mdogo na hivyo kuionba serikali kuipatia fedha kwa ajili ya kujenga mabwawa mapya ya kutibu maji hayo.