23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkenda apinga agizo la Mrajis kufuta vyama 32

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

WAZIRI wa Kilimo, Profesa Aldof Mkenda amepinga agizo la Mrajis Mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini lakufuuta Muungano wa yama 32 vya msingi vya Ushirika ambavyo mwaka 2003 vilijiondoa kutoka Chama Kikuuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU) na kwamba  ushirika ni hiari  na siyo lazima.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Desemba 13, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa bodi ya kahawa Tanzania (TCB) mjini Moshi mkoani Kilimanjaro nakuhudhuriwa wadau wa kahawa kutoka Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) na wawakilishi kutoka Chama Kikuu cha Ushirika KNCU.

Amesema ushirika ni hiara na siyo lazima, hivyo KNCU wanatakiwa kuboresha mazingira ili vyama vya ushirika vya msingi vione faida ya kurudi na siyo kuwalazimisha na kuwatishia hilo ni kosa.

“Hatuwezi kuwalazimisha watu kuungana kwa nguvu na ikumbukwe ushirika ni hiari siyo lazima pia umoja ni nguvu, hivyo KNCU mrejeshe imani kwa wakulima waone manufaa ya kurudi KNCU bila hivyo ni vigumu, nisingependa kuona mtu anatoa amri kwa vyama hivyo kuungana kwa nguvu,” amesema Prof. Mkenda.

Itakumbukwa, hivi karibuni Mrajis  wa vyama vya Ushirika nchini alitangaza kuufuta muungano wa vyama 32 vya msingi vya ushirika ambavyo mwaka 2003 vilijiondoa rasmi kutoka Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU 1984)Ltd.

Kupitia tangazo la serikali (GN) Na.725 na barua yake yenye Kumb.Na. CLA/69/186/01/07 ya juni 8, 2020, mrajis ameelekeza shughuli zote za ukusanyaji wa kahawa kutoka kwa wakulima zilizokuwa zinafanywa na G32 sasa zihamishiwe KNCU.

Shughuli hizo ni pamoja na kahawa ambayo tayari ipo mikononi mwa muungano huo kutoka kwa wakulima ambayo haijauzwa nayo ikabidhiwe kwa KNCU ili taratibu za kuiuza zifanywe na chama hicho kikongwe china.

Aidha, Prof. Mkenda amesema anashangaa kuona mtu kutumia nafasi yake vibaya bila hoja za msingi na kwamba huko ni kuwadidimiza wakulima.

 “Nitakwenda kukaa na watalaamu kufuatilia kwa kina hili suala la G 32 nitakuja kulitolea majibu sahihi, “amesema.

Prof. Mkenda amesema iwapo wahusika wa vyama hivyo wasipofanyakazi wataviua vyama hivyo na ushirika kwa ujumla.

Katika barua yake Mrajis alitaja moja ya sababu ya kufuta vyma hivyo kuwa ni kufanana kwa shughuli zinazofanywa na muungano huo na zile zinazofanywa na KNCU huku akieleza kuwa wanachama wa G32 ni wanachama pia wa KNCU.

Aidha, muungano huo unaojulikana kama Kilimanjaro New Co-Operative Initiative Joint Venture (G32 KNCI-JVE Ltd), umekuwa mhimili mkubwa katika kusimamia ukusanyaji wa kahawa kutoka kwa wakulima waliopo chini ya mradi huo ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi.

Muungano huo ulibuniwa msimu wa 2002/2003 baada ya sheria ya ushirika na ile ya kahawa kubadilishwa mwaka 1994 hivyo kuruhusu wakulima kuuza mazao yao ikiwamo kupitia ushirika au kwa watu/makampuni binafsi pamoja na sheria mpya kuruhusu soko huria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles