23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwana FA aanza kutekeleza ahadi Muheza

Na Amina Omari, Tanga

Mbunge wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amechangia matofali 1,050 pamoja na fedha Sh milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Kwa Mkabala,

Msaada huo ameutoa jana Desemba 13, wakati wa zoezi la kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo ambapo amesema kuwa msaada huo utasaidia kikamilisha chumba kimoja cha darasa.

Amesema shule hiyo ambayo ilikuwa na madarasa matatu tuu hali iliyokuwa ikisababisha wanafunzi kulazimika kwenda shule ya jirani ya Masuguru.

“Nimekuja leo kutimiza sehemu ya ahadi yangu wakati wa kampeni za Kugombea Ubunge ambapo niliahidi kushirikiana na Wananchi kujenga Darasa la nne mwezi huu wa 12 ili Watoto waweze kuendelea na masomo yao hapa hapa,” amesema Mwijuma.

Amesema kuwa shule hiyo ambayo ina idadi ya watoto 3000 inakabiliwa uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa 72 hali ambayo inatishia utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles