Peter Fabian na Raphael Okello-Nansio/Ukara
MUUJIZA. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mhandisi Mkuu wa Kivuko cha MV Nyerere, Alphonce Charahani, kuokolewa akiwa hai licha ya kukaa ndani ya maji kwa saa 44 tangu kilipopinduka na kuzama Alhamisi wiki hii saa nane mchana katika Ziwa Victoria wakati kikitokea Kisiwa cha Bugolora kuelekea Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, huku kikidaiwa kubeba idadi kubwa ya abiria na mizigo mingi kuliko uwezo wake.
Alphonce aliokolewa jana saa 4:45 asubuhi akiwa hoi katika chumba cha injini (ghamla) kilichokuwa juu baada ya kivuko hicho kuzama huku mwili wake ukiwa umelowa mafuta mazito (oil) na alisikika akiomba kupewa chai au maji ya kunywa.
Alipoulizwa endapo kama kulikuwa na watu wengine ndani ya kivuko hicho katika eneo alilokuwapo, alitoa ishara ya kukataa akimaanisha hakuwa akielewa zaidi na timu ya wataalamu waliokuwa wanaokoa watu walishauri aachwe apumzike ili aweze kutoa maelezo mazuri zaidi baadaye.
Kuokolewa kwa Alphonce kunaongeza idadi ya wafanyakazi wa kivuko hicho kufika watatu, wa kwanza akiwa ni Nahodha msaidizi, Frances Mayagi na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Gombo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (DCP) Jonathan Shanna, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na alisema wanadhani Alphonce ndiye aliyekuwa akigonga ndani ya kivuko hicho tangu siku ya kwanza ilipozama na kwa sasa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Bwisya Ukara.
Pia alisema inaaminika Alphonce alikuwa ndani ya chumba cha injini ambacho wakati mwingine …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA