29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mhagama: Sekta ya Kazi na Ajira fanyeni kazi pamoja

Na Faraja Masinde, Mbeya

Serikali imezitaka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Wakala wa Usalama mahala pa Kazi (OSHA) kufanyakazi kwa kushirikiana ili kusaidia kusukuma maeneo ya Taifa mbele.

Wito huo umetolea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama wakati wa hafla ya kukabidhi vitendea kazi 10 (Kompyuta) kwa Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Shanes Nungu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Mbeya ili kuharakisha shughuli za usuluhishi wa migogoro ya kazi.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (wapili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Shanes Nungu (wapili kushoto) moja kati ya kompyuta 10 zilizotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Novemba 29, 2021 jijini Mbeya. Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Kaspar Muya (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk. John Mduma.

Amesema ushirikiano ndio utakao saidia kuskuma maendeleo ya taifa mbele na kwamba itakuwa rahisi hata kushughulikia changamoto pale zinapojitokeza.

“Hii kwangu ni habari njema na kuona kwamba WCF inakwenda kuiwezeaha CMA kutekeleza majukumu yake kwa urahisi, hivyo niwashukuru wote kwa kuona kuwa mmoja anatambua changamoto za mwenzake.

“Hivyo niendelee kusisitiza kuwa sekta ya kazi na ajira muendele kufanyakazi pamoja ili taifa letu lisonge mbele,” amesema Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amewashukuru wa kuu wa WCF na CMA kwa kuona umuhimu huo wa kushirikiana.

“Kipekee napenda kuwashukuru sana sana wakuu wote na viongozi wa taasisi zote Dk. John Mduma Mkurugenzi Mkuu wa WCF na kaka yangu Nungu Mkurugenzi Mkuu wa CMA kwa kuona umuhimu wa kufanya kazi kama serikali moja, ninyi wote mko chini ya mwamvuli mmoja, ili kuhakikisha kwamba mmoja anapogundua changamoto ya mwenzake anaamua kusimama naye na kuweza kumsaidia,” amesema Waziri Mhagama.

Aidha, ameongeza kuwa, WCF imekuwa ikifanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake tangu uanzishwe miaka sita iliyopita, sheria iliyokuwepo kabla ya kupata uhuru, mfanyakazi alikuwa akiumia analipwa Sh 108,000 haijalishi awe amepata ulemavu wa aina gani malipo ya fidia yalikuwa ni flat rate.

“Mwaka 2008 Sheria ilifanyiwa marekebisho ambapo mwaka 2015 tuliunda Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umechukua jukumu la Fidia, kuhangaika na magonjwa na madhara yatokanayo na kazi kutoka kwa waajiri na kuwekwa kwenye Mfumo maalum na sasa uko kwenye Mfuko wa WCF,” amesema Mhagama.

Ameongeza kuwa katika muktadha huo huo wa kuhakikisha serikali inayagawa majukumu kiutendaji na kisheria ilianzisha CMA ili taasisi hii ishughulike na masuala ya usuluhishi na uamuzi inapotekea migogoro ndani ya maeneo ya kazi.

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akipokea Kompyuta kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk. John Mduma ambazo zilitolewa na Mfuko kuisapoti CMA.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dk. John Mduma amesema, makabidhiano hayo ya computer ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mhagama aliyetaka taasisi hizo zifanye kazi kama ndugu.

“Kwa kufanya kazi kwa pamoja ndipo tunaweza kufikia malengo yetu kama taasisi lakini kwa pamoja kama ofisi yako Mheshimiwa Waziri, tunatambua kwamba mmoja wetu kama atakimbia mbio na uwezo wake alionao na akawaacha ndugu zake nyuma, hatatoboa yeye peke yak,” amesema Dk. Mduma.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Shanes Nungu amemshukuru Waziri Jenista kwa maono yake na kuwezesha CMA kupata msada huo wa kompyuta.

“Mheshimiwa Waziri nakumbuka ulisema nyie watoto sita kwanza shikamaneni halafu saidianeni na agizo lako limezaa matunda, sio mara ya kwanza kwa WCF kutusaidia mara ya kwanza walitusaidia computer kumi ambazo zilisaidia kutatua malalamiko ya wananchi kucheleweshewa hukumu zao kupungua,” amesema Nungu.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge), Kaspar Muya, wakurugenzi wa WCFna CMA pamoja na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni NSSF, PSSSF, OSHA na Idara ya Kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles