26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mgombea urais 2015 atinga Vatican

Mtanzania
Mtanzania

NA MWANDISHI WETU

WAKATI joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 likiendelea kupanda miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaohusishwa na harakati za kuwania urais, mmoja wa makada hao amekwenda Vatican kwa nia ya kutafuta uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki duniani, MTANZANIA Jumapili limedokezwa.

Habari za uhakika kutoka katika chanzo cha karibu na kada huyo ambaye pia ni waziri kwenye moja ya wizara nyeti nchini, kimedai kuwa waziri huyo amezuru jijini Vatican hivi karibuni.

Mtoa habari wetu huyo alilidokeza gazeti hili kuwa licha ya ziara ya waziri huyo jijini Vatican kuonyesha kuwa ni ya kikazi, lakini lengo kuu la kuelekea huko lilikuwa ni kutambulisha dhamira yake ya kuwania urais 2015.

Alisema kuwa waziri huyo, ambaye katika historia ya elimu inaonyesha amepata kusoma shule ya seminari, alipofika mjini Vatican alikutana kwa faragha na maofisa kadhaa wa Kanisa Katoliki duniani, ambapo alitumia nafasi hiyo kupenyeza lengo lake kuhusu dhamira ya kugombea urais mwakani.

“Alikwenda Vatican akiwa na lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Kanisa Katoliki na tangu amerudi amekuwa akijinadi kwamba Vatican itamuunga mkono Rais wa Tanzania mwaka 2015,” alisema mtoa habari wetu huyo.

Awali gazeti hili lilidokezwa na chanzo kingine cha habari ambacho kipo naye karibu katika wizara anayoiongoza kuwa waziri huyo alisafiri kwenda Vatican mwishoni mwa Julai na akarejea nchini mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu.

Mbali na ziara ya Vatican, waziri huyo amedaiwa kuwa na mpango wa kukutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini, Kardinali  Polycarp Pengo, kwa lengo la kumdokezea juu ya dhamira yake hiyo, hasa baada ya kuwa amerudi kutoka makao makuu ya kanisa hilo.

Katika hatua nyingine, gazeti hili lilimkariri mmoja wa vijana anayeunda kundi linalompigia kampeni waziri huyo akisema: “Tayari tupo vijana ndani ya CCM ambao tumeanza kuzunguka nchi nzima kueneza habari hii ya mavuno kwetu”.

Pia kijana huyo alidokeza kwamba hivi karibuni waziri huyo ameingiza nchini magari 24 aina ya VX Land Cruiser kutoka katika nchi za Falme za Kiarabu kwa ajili ya kuendesha mkakati wa kundi lake wa kuzunguka nchi nzima kutafua ushawishi ndani na nje ya chama.

Kijana huyo alidai kwamba moja ya magari hayo analitumia mmoja wa viongozi wa juu wa CCM ambaye hivi karibuni alikwenda nalo mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya Kamati Kuu ya chama (CC).

Waziri huyo anayetajwa katika mikakati ya sasa ni mmoja kati ya makada sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanatumikia kifungo cha mwaka mmoja cha kutojihusisha na masuala ya siasa kwa kosa la kuanza kampeni za urais mapema kinyume cha kanuni za chama.

Wanaotumikia adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward, Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira.

Wengine ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

- Advertisement -

Related Articles

12 COMMENTS

    • Nawapongeza wote wanaojinadi na kujitokeza mapema katika kinyang’anyiro cha kugombea urais wa 2015 hii inatusadia sisi tutakaopiga kura kuwajua, kuwafuatilia,kuwapima na kujua mapema yupi anafaa na yupi hafai.Sioni sababu ya kuwazuia wakati ukifika mbivu na mbichi itaonekana wazi.Kumbuka nyota njema huonekana asubuhi.Waacheni wajinadi watajichambua wenyewe na anayefaa atajulikana na kung’ara bila kujificha.

  1. Hii ni njia ya kuharibu sifa ya Mtanzania yeyote wa dini yeyote ile na pia kwa wale wasio na dini. Uchochezi kama huu siyo mzuri kwa manufaa ya taifa la Tanzania. Kuandika nakala za kuelimisha ni nzuri kuliko nakala za uchochezi na uzushi.

  2. Siyo suala genihili kwa watanzania huko nyuma kuna Kiongozi mmoja Mkristu aliishaenda nchi za Uarabuni akitaka kuungwa mkono na akabadili jina na kuitwa Jumanne. Hata huyo aliyeenda Vatican mwache aende akiungwa mkono na chama chake kuna ubaya gani!! Wangapi wanaenda Bagamoyo wakati wa chaguzi za hapa Tanzania. Suala la msingi ni uwezo wa kuongoza nchi hii iliyojaa viongozi Mafisadi.

  3. To be frank mimi sioni mantiki ya hii habari, kuna dhambi gani mtu kwenda huko na kutaka baraka kama ndo hivyo! Bora huyo aloenda vatican kuliko waaoenda kwamsangoma

  4. Kama Watanzania watamhitaji hakukuwa na sababu ya kwenda Vatican, Vatikani haiongozi Tanzania wala haijapewa udhamini, Tanzania ni ya Watanzania wenyewe. Vatican ikimwunga mkono itamsaidia nini, haitaweza kuwalazimisha Watanzania zaidi ya milioni 45 wamchague mtu huyo!. HUKO NI KUTAPATAPA NA KUTOKUJUA LA KUFANYA.

  5. Sioni ni kwa nini mwandishi ameharakisha habari hii kabla hajaweza kuwa wazi na habari yake. Amtaje ni waziri gani, ili na sisi tuweze kujua kweli ziara yake inapaswa kuhusishwa na kutaka uungwaji mkono na Vatican au na wewe unatumiwa na wagombea wengine kutaka kuwaharibia wengine? Suala la kumpata rais ni la watanzania na wala siyo la Vatican wala Marekani!!

    • halo umenena Julius. maana sisi ndio we ye nchi name kura. Pinda anakimbilia Vatican ili Papa amwamuru Pengo atoe amri au afanyeje. papa hata hajui Hindi CCM wanavyotufanyia. pinda ni mhuni kwa sababu amejua Kuwait wakatoliki ni wengi sasa anatugiribu kama watoto. pinda acha utoto tumeshakua Mzee.

  6. CCM wanahaha, wanataka kutudanganya name sasa wanaona tamko la maaskofu limewabana. sasa anakimbilia Vatican kutafuta kura za wakatoliki. issue siyo Vatican ishu kubwa ni kwamba CCM itatufikisha Kule tunakotaka kwenda? ikiwa tu eneo la katiba wameshindwa kututendea khaki watanzania je itakuwaje tuwape kura zetu?. tena ni afadhali kama angekuwa mwingine lakini Pinda! mhmmm afadhali hata ya LOWASA ningefikiria

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles