25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyakazi awaambukiza corona wafanyakazi 533

ACCRA, GHANA

MFANYAKAZI mmoja wa kiwanda cha samaki nchini Ghana, amewaambukiza kirusi cha corona kinashosababisha maradhi ya Covid-19 wafanyakazi wenzake 533 wa kiwanda hicho.

Hayo yameelezwa na Rais Nana Akufo-Addo katika hotuba kwa taifa jana na kusisitiza kuwa, watu wote hao 533 waliambukizwa virusi vya corona na mtu mmoja. 

Hata hivyo hakutoa ufafanuzi ni vipi  ugonjwa huo wa Covid-19 ulienea kiwandani humo na kama hatua za tahadhari za kiafya zimechukuliwa kufuatia maambukizi hayo.

Kwa mujibu wa Rais Akufo-Addo, maambukizi hayo ya watu 533 waliothibitika kuwa na virusi vya corona, ikiwa ni takribani asilimia 11.3 ya maambukizo yote ya nchi nzima ni sehemu ya kesi mpya 921 za watu waliobainika kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 katika kipindi cha karibu wiki mbili zilizopita ambazo takwimu zake zimetolewa hivi karibuni.

Katika hotuba yake hiyo ya jana, Rais wa Ghana alirefusha tena marufuku ya mikusanyiko ya umma hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Mei huku shule na vyuo vikuu nchini humo vikiendelea kufungwa.

Mamlaka za Afya za Ghana ziliripoti siku ya Ijumaa kuhusu mripuko huo wa maambukizo ya corona katika kiwanda hicho cha samaki kilichoko kwenye mji wa kando ya bahari wa Tema lakini hazikutoa maelezo zaidi.

Maambukizo mapya ya corona yaliyotangazwa jana yameifanya Ghana kuwa na jumla ya watu 4,700 wenye virusi vya corona tangu mripuko wa janga hilo lililoikumba dunia nzima ulipotangazwa nchini humo kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Machi.

Takwimu za jana zimeifanya Ghana kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi vya corona katika eneo la Afrika Magharibi.

Hadi sasa watu 22 wamefariki dunia kwa maradhi ya Covid-19 nchini humo na wengine 494 wamepata afueni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles