24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Manara anyoosha mikono kwa Senzo

Na WINFRIDA MTOI

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameshindwa kuzuia hisia zake na kumtaja bosi wake, Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O), kuwa ni kati ya viongozi wachapa kazi.

Senzo raia wa Afrika Kusini, aliyetua nchini mwaka jana, amekuwa nyuma ya mafanikio ya Simba msimu huu ambayo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 71.

Katika ukurasa wake wa instagram wakati wa kumtakia heri ya kuzaliwa, Manara, aliandika kuwa, kwa miezo saba aliyokaa na Senzo, amejifunza mambo mengi kutokana na kiongozi huyo kulifahamu vizuri soka la Afrika.

Manara alisema amegundua kuwa CEO huyo, yupo makini katika kufanya kazi yake inavyotakiwa pia ana ushirikiano mkubwa na watu wanaomzunguka ndani na nje ya kazi.

“Kwa miezi saba niliyofanya kazi na huyu mtu (Senzo), nimegundua na kujifunza vitu vingi sana, jamaa anajua soka na utawaka wake, ana ushikiano  katika kazi na nje ya kazi.

 “Ni mtu muungwana na hodari kusoma mazingira, hakika Simba imepata mtu sahihi kwa nafasi ya C.E.O wa klabu,” alisema Manara.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,249FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles