33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Iran yawaua kimakosa wanajeshi 19

TEHRAN, IRAN

WANAMAJI 19 wameuawa na wengine 15 wakajeruhiwa katika tukio la ajali lililohusisha meli za kijeshi za Iran katika Ghuba ya Oman, jeshi la Iran limesema.

Vyombo vya habari vya Iran vilisema kwamba meli hiyo kwa jina Konarak ilishambuliwa na kombora jipya lililokuwa likijaribiwa na meli ya kijeshi ya Frigate Jamaran wakati wa zoezi la kijeshi siku ya Jumapili.

The Konarak ilishambuliwa na kombora jipya Jumapili mchana wakati wa zoezi la kijeshi katika maji ya Bandar-e Jask Kusini mwa Pwani kulingana na runinga ya taifa katika tovuti yake.

Wanamaji hao walisema meli hiyo ilivutwa hadi ufukweni na kwamba uchunguzi umeanza.

Kisa hicho kilitokea karibu na mkondo wa bahari ya hormuz, eneo muhimu la kimkakati ambapo kiwango kikubwa cha mafuta duniani hupitia.

Mwezi Januari , kitengo cha ulinzi wa angani kilirusha kumbora kutoka ardhini kikilenga kitu kisichojulikana, hatua ilioangusha ndege ya kampuni ya Ukrain na kuwaua wote waliokuwa wakiabiri ndege hiyo.

Makosa hayo yalifanyika wakati wa hali ya wasiwasi huku Iran ikisubiri kombora la kulipiza kisasi kutoka kwa Marekani.

Lakini tukio hilo la siku ya Jumapili lilifanyika katika hali tofauti wakati wa zoezi la wanamaji na linaibua maswali mengi kuhusu uongozi na udhibiti na utaalam wa jeshi la wanamaji wa Iran.

Iran inataka kupanua operesheni zake na kuimarisha silaha katika meli zake, Frigate Jamaran ambayo ni miongoni mwa vyombo vilivyoundwa nchini humo ikitarajiwa kuweka rekodi mpya.

Lakini ni jeshi lisililotiliwa maanani . Ni jeshi la wanamaji wa Revolutionary Guard lenye boti zinazopiga doria katika eneo hilo ambalo linahusika mara kwa mara katika kuhangaisha na kuchunguza meli za Marekani na nyenginezo katika Ghuba hilo.

“Siku ya Jumapili jioni…wakati wa zoezi la wanamaji ambalo lilihusisha vyombo kadhaa vya wanamaji katika maji ya Jask and Chabahar , tukio moja lilifanyika likihusisha meli ya Konarak , na kuwaua baadhi ya wanajeshi jasiri wa jeshi hilo, wanamaji hao,” walisema katika taarifa jana.

Taarifa hiyo iliongezea kwamba meli hiyo ya Konarak ilikuwa imepelekwa katika bara moja kwa uchunguzi wa kiufundi, lakini haikutaja tukio la ajali hiyo.

Vyombo vya habari vya Iran awali vilikuwa vimeripoti kwamba meli ya Konarak ilishambuliwa kwa bahati mbaya na kombora moja lililifyatuliwa kutoka katika meli.

Meli hiyo ilishambuliwa baada ya kupita katika eneo ambalo kombora hilo lilikuwa likirushwa baada ya kushindwa kupita mbali, runinga ya serikali ilisema katika tovuti yake.

Chombo cha habari cha Tasnim kilituma ujumbe wa twitter kwa kiingereza kwamba Konarak ilizamishwa katika tukio hilo.

Kiliripoti kwamba meli hiyo iliharibiwa vibaya. Haijulikani kulikuwa na wanamaji wangapi ndani yake wakati huo.

Meli ya kivita ya Konarak ina urefu wa mita 47 na ilitenegenezwa nchini Uholanzi na kununuliwa na Iran kabla ya mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles