24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara aficha mwanamke ndani ya shimo

FuimeNa Asifiwe George, Dar es Salaam

MFANYABIASHARA maarufu wa mabasi ya kwenda mikoani anadaiwa kumficha mwanamke ndani ya shimo kwa   zaidi ya mwaka mmoja.

Tukio hilo liligundulika  Mbezi Luis  Dar es Salaam jana, ambako ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa amefichwa ndani ya shimo linalokadiriwa kuwa na urefu wa futi 10.

Kwa majibu wa mshuhuda wa tukio hilo,   mmoja wa wapita njia alisikia sauti ya mtu ikitoka katika shimo lililokuwa jirani na nyumba ya mmiliki huyo wa mabasi na  kuwaita watu waweze kushuhudia.

“Hili tukio ni la aina yake… inaelekea huyo dada yumo ndani ya hili shimo kwa zaidi ya mwaka, tena alikuwa akila unga maana mwili wake umedhoofika sana,” alisema mmoja wa mashuhuda ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini.

Vilevile, picha ya video ya mwanamke huyo zilionekana katika  mitandao ya jamii jana zikimuonyesha  akiwa mtupu.

Video hiyo iliwaonyesha   polisi wakimuhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa ajibu maneno yasiyoeleweka mithili ya mgonjwa wa akili.

Picha hizo zilikuwa zikimuonyeha mwanamke huyo akiwa anacheka na kuficha sura yake ili asionekane kwa watu waliokuwa katika eneo hilo, huku akiwa anajilaza chini na kuinuka.

Askari hao kwa kushirikiana na wananchi waliweza kumtoa ndani ya shimo hilo na kumpakia ndani ya gari kabla ya kumpeleka katika Kituo cha Polisi Mbezi.

Mmoja wa maofisa wa polisi wa Kituo cha Mbezi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

“Tukio hilo ni la ukweli na hata picha zipo zimesambazwa katika mitandao ya jamii zikionyesha kilichotokea,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi wa Konondoni, Christopher Fuime alipotafutwa alikanusha kuwapo  tukio hilo.

“Ndugu mwandishi sina taarifa ya mwanamke aliyekutwa uchi,” alisema Kamanda Fuime kabla hata ya kuulizwa swali lolote na mwandishi .

Mwandishi  pia  alimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,  Simon Sirro, ambaye   alisema kuwa ndiyo alikuwa analisikia suala hilo  kupitia kwa mwandishi.

Hata hivyo alisema angewasiliana  na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni  kujua ukweli wa tukio hilo.

“Kwa kweli mimi sina taarifa hiyo wala hizo picha sijaziona, taarifa hii ndiyo naisikia kwako.  Ngoja nitoe maagizo  kwa RPC  wa Kinondoni   afuatilie tukio hilo   kuweza kupata uhakika  wa jambo hilo,” alisema Kamanda Sirro.

Baada ya saa moja MTANZANIA ilimtafuta tena Kamanda Fuime   kujua kama alikuwa amekwisha kuzipata taarifa  taarifa za tukio hilo lakini  alisimamia kauli yake ya awali kwamba halikuwapo tukio lolote la mwanamke kukutwa shimoni Mbezi Luis.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles