27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mez B kuzikwa Dodoma leo

Mez-BNA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

MWILI wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moses Bushagama ‘Mez B’, unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya wahanga wa treni, Mailimbili mkoani hapa.

Mez B alifariki dunia Ijumaa ya wiki iliyopita, mjini hapa wakati akiwaishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akidaiwa kuugua ugonjwa wa Pneumonia.

Akizungumza na MTANZANIA jana mjini hapa, mama mzazi wa marehemu, Merry Katambi, alisema mwanaye atazikwa leo katika makaburi hayo ya wahanga wa treni.

Alisema mwili wa marehemu utaagwa katika Viwanja vya Nyerere Square, mjini hapa kuanzia majira ya saa saba mchana, huku ibada ya kumuombea nayo ikifanyika katika viwanja hivyo.

“Mwanangu tutamzika Jumatatu (leo) katika makaburi ya wahanga wa treni Mailimbili, ila ibada pamoja na kuuaga mwili wa marehemu zitafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere,” alisema.

Mez B alikuwa ni mwanzilishi wa Kundi la Chemba Squad la mkoani hapa, akiwa pamoja na Dark Master, Noorah na marehemu Albert Mangwea, huku akitamba na baadhi ya nyimbo zake kama Kikuku cha Mama Rhoda na Nimekubali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles