25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Messi aongoza kifedha, Ronaldo wa pili

PARIS, UFARANSA
KWA mujibu wa mtandao wa Goal, nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi, ametajwa kuwa mchezaji anayeongoza kwa kuwa na pato kubwa la fedha kwa mwaka kuliko mchezaji yeyote duniani.

Messi anaongoza kwa kipato akifuatiwa na mpinzani wake, Cristiano Ronaldo, wanayelingana naye kwa tuzo tano za Ballon d’Or kila mmoja.
Mapato ya wachezaji hao yanatokana na mshahara wanaolipwa na klabu wanazozitumikia, bonasi, fedha za matangazo na mambo mengine mengi yanayowaingizia fedha kwa mwaka.

Messi anaongoza huku akiwa anaingiza kiasi cha pauni milioni 145 kwa mwaka, ambazo ni zaidi ya bilioni 437 za Kitanzania, wakati Ronaldo akiingiza pauni milioni 97 kwa mwaka, zaidi ya bilioni 292 za Kitanzania.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr, ambaye anachukua kiasi cha pauni milioni 79, ambazo ni zaidi ya bilioni 238 za Kitanzania na nafasi ya nne inashikiliwa na nyota wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Antoine Griezmann anayeingiza pauni milioni 38 ambazo ni zaidi ya bilioni 114.

Namba tano inashikiliwa na mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale ambaye anaingiza kiasi cha pauni milioni 34.5 zaidi ya bilioni 103. Nyota wa zamani wa Barcelona, Andres Iniesta ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Vissel Kobe huko nchini Japan, anaingiza kiasi cha pauni milioni 28.3 zaidi ya bilioni 85.

Wachezaji wengine wanaoingiza wanaofuata kwa kuingiza kipato zaidi ni Alexis Sanchez kutoka Man United, anayeingiza pauni milioni 26.3 zaidi ya bilioni 79. Philippe Coutinho anaingiza pauni milioni 25.7 zaidi ya bilioni 76. Ezequile Lavezzi anayekipiga timu ya Hebei China Fortune, anaingiza pauni milioni 24.3 huku Luis Suarez akiingiza pauni milioni 24.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles