28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Meridianbet Mkuchu Cup Imehitimishwa Kwa Matembezi ya Hisani!

Tunarudisha Kwenye Jamii Inayotuzunguka.

Meridianbet kwa kushirikiana Emanuel Mkuchu (muandaaji wa Meridianbet Mkuchu cup) pamoja na Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama,  walishirikiana kuandaa matembezi ya hisani yaliyoambatana na ufanyaji usafi wa zahanati ya Kunduchi ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa tiba na vifaa vya usafi wa ndani na nje ya zahanati hiyo.

Zoezi hilo lililofanyika Februari 26, 2022, lilihuduliwa na viongozi mbalimbali wa eneo la Kunduchi akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtongani, Bwana Tabu Athumani pamoja na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilongawima, Bwana Emmanuel Mkuchu.

Akiongea na waandishi wa habari, Bwana Tabu Athumani alisema, “Kwa dhati kabisa nimshukuru mwanzilishi wa hili wazo la kufanya hisani hii ndani ya zahanati iliyopo katika eneo langu lakini kubwa zaidi, Meridianbet kwa kuhakikisha inasaidia vifaa hivi vya usafi kwenye zahanati yetu inayohudumia karibu kata nzima ya Kunduchi. Ninawatakia heri kwenye kukamilisha mashindano yenu hapo badae na Mungu awatangulie”

Afisa Masoko wa Meridianbet Tanzania, Bwana Twaha Ibrahim amesema, “lengo la Meridianbet ni kuijulisha jamii kuwa michezo ni fursa kwa vijana na chachu ya ushirikiano na wao (Meridianbet) wapo tayari kuwa sehemu ya kuhamasisha na kuhakikisha michezo inakua sehemu ya kipato kwa vijana na jamii kwa ujumla” .

Meridianbet Mkuchu Cup imechukua taswira hii kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya kata ya Kunduchi na sehemu mbalimbali za Dar es salaam.

“Vijana ni nguvu kazi ya taifa, na wanavipaji sana lakini, baadhi yao bado hawajaonekana vyema kwenye tasnia ya soka. Michuano hii inawapa nafasi ya kuonekana kwa jamii na kujipatia fursa ya ajira. Pia, hii ni burudani kwa wananchi wanaohudhuria michuano hii.” Alizungumza Emmanuel Mkuchu, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kilongawima, ambaye ni mratibu wa michuano hii kwa kushirikiana na Meridianbet.

Fainali ya michuano hii ilifanyika Februari 26, 2022 ambapo ilihudhuriwa na Meya wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Songolo Mnyonge ambapo, Tanga Boys waliibuka washindi na walijishindia pikipiki aina ya Tvs King yenye thamani ya shilingi millioni 2.6 na kukabidhiwa zawadi yao na mgeni rasmi. Mshindi wa pili walikua ni Nondo FC ambao walijishindia Milioni 1 taslim, wakati mchezaji bora wa mashindano hayo akipata shilingi laki 1.
 

Meridianbet Pekee, Mabingwa Ndio Nyumbani Kwao!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles