Kampuni ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet kwa kushirikiana na Global Peace Foundation Tanzania zimeadhimisha siku ya mazingira duniani kwa kusafisha soko la Tandale na kupanda miti ya kivuli na matunda kwenye hospital ya eneo hilo, Dar es Salaam.
Tukio hilo limeanza saa 12 asubuhi kwa watumishi wa kampuni hiyo kufanya katika maeneo mbalimbali kuzunguka soko la Tandale na kisha kupanda miti ya kivuli na matunda kwenye hospitali ya Tandale.
Mkuu wa kitengo cha ustawi wa jamii cha Meridian Bet, Amani Maeda amesema kampuni yao inaungana na mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku ya mazingira.
“Mazingira ni watu na watu ni mazingira, bila mazingira kuwa safi, hatuwezi kuwa na jamii yenye afya, ndio sababu Meridian Bet tumeungana na wenzetu wa Global Peace Foundation Tanzania kufanya usafi na kupanda miti katika kuadhimisha siku ya mazingira,” amesema Amani.
Naye msimamizi mkuu wa maduka ya Meridian Bet Dar es Salaam na Pwani, Seif Simba amesema wameshiriki katika maadhimisho hayo kwa kufanya usafi katika soko na kupanda miti hospital kwani maeneo hayo yanahudumia jamii kubwa.
“Kama kawaida yetu Meridian Bet kushirikiana na jamii, ndiyo sababu tumeadhimisha siku ya mazingira kwa kusafisha soko la Tandale na kupanda miti kwenye hospitali,” amesema.
Ofisa programu wa Global Peace Foundation Tanzania, Benson Daudi amesema zoezi hilo litakuwa endelevu.
“Tutaendelea kufanya usafi na kupanda miti katika maeneo mbalimbali yanayohudumia jamii hata baada ya maadhimisho haya,” amesema Daudi.