24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Membe ‘out’ CCM, Kinana apewa karipio, Makamba asamehewa

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemfukuza uanachama aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Bernard Membe kwa kukiuka maadili ya chama.

Aidha, kamati hiyo imetoa karipio kwa Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kwa kukiuka maadili ya chama huku ikimsamehe Yusuph Makamba kwa makosa kama hayo.

Uamuzi huo umetangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo Ijumaa Februari 28, jijini Dar es Salaam.

“Kamati Kuu wa CCM kwa kauli moja imeazimia kwamba Membe afukuzwe uanachama wa CCM, uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonyesha mwenendo wake tangu mwaka 2014 ambapo kwenye chama ameshawahi kupata adhabu nyingine ambazo zingemsaidia kujirekebisha lakini imeonekana sivyo.

“Aidha, kamati kuu imepokea maelezo ya Kinana na imeazimia apewe adhabu ya karipio kwa mujibu kanuni za chama,” amesema.

Kuhusu Makamba, Polepole amesema baada ya kufuatilia kwa kina kumhoji na kumsikiliza na kufuatilia mwenendo wake kamati kuu imeazimia Mzee Makamba asamehewe.

“Wakati wote tangu aliposomewa mashtaka yake amekuwa mtu muungwana, mnyenyekevu na mtii kwa mamlaka ya chama na ameomba asamehewe makosa yake kwa barua na amesamehewa makosa yake.

“Adhabu ndani ya CCM zinaweza kuwa siri akaambiwa mhusika au zikawa za wazi, adhabu ya karipio inasomwa hadharani na kufukuzwa inasomwa hadharani,” amesema Polepole.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles