27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mwanamke aolewa na wanaume wawili Nigeria

Kano, Nigeria

MGOGORO mkali wa kimapenzi umeibuka katika jimbo la Kano nchini Nigeria ambapo wanaume wawili wamemuoa mwanamke mmoja kwa wakati tofauti.

Katikati ya mgogoro huo ni mwanamke aliyetajwa  kwa jina Hauwa Ali Mariri mwenye umri wa miaka 32 ambaye sasa anahofia adhabu iwapo atapatikana na hatia ya kuwadanganya wanaume hao.

Kano ni mojawapo ya majimbo kadhaa ya Nigeria ambayo yanaongozwa kupitia sheria ya Kiislamu na ni makosa kwa mwanamke kuolewa zaidi ya mwanamume mmoja.

Mambo yalibadilika na kuwa mabaya wakati Bello Ibrahim mwenye umri wa miaka 40, mume wa kwanza wa Mariri aliporudi nyumbani na kumkuta mwanamume mwingine amelala katika kitanda chake.

Ibrahim alikuwa ameugua kwa muda mrefu na alikua amesafiri kijijini ili kupata matibabu ambapo alikaa huko kwa takriban miaka miwili.

Anamtuhumu Mariri kwa kufunga ndoa bila yeye kujua. Lakini aliiambia BBC kwamba walitalakiana.

”Alisema  ameniacha kabla hajaenda kijijini. Ndio maana nilifunga ndoa na Bala, nilihisi kwamba nilikuwa huru aliposema kwamba amenipa talaka”, alisema.

Hatahivyo Ibrahim amekana hilo akisema hakumpa talaka na kwamba bado anamchukulia kama mkewe.

Ibrahim na Mariri walioana takirban miaka 17 na wakajipatia watoto sita.

”Sikumuacha. Iwapo anasisitiza kwamba nilimpa talaka ushahidi uko wapi, barua niliyomuandikia iko wapi?”,

Talaka nyingi nchini Nigeria hutolewa kwa mdomo ama kupitia barua.

Ibrahim aliyevunjika moyo aliwasilisha malalamishi yake kwa polisi wa jimbo hilo ambapo kisa hicho kinachunguzwa na wote watatu wamechunguzwa.

Bala Abdulsalam mwenye umri wa miaka 35 ,mwanamume wa pili alisema kwamba Mariri alimwambia kwamba alikuwa ameachana na mumewe na kwamba alikuwa tayari kufunga naye ndoa.

Anasema alimtumia dola 50 za Marekani kusimamia ndoa hiyo pamoja na mahari.

”Nilikuwa nje ya mji wakati nilipomtumia fedha hizo, niliporudi Kano alikuwa mke wangu”, aliambia BBC.

Anahofia kuadhibiwa iwapo mahakama za sheria zitamkuta na hatia za kumuoa mke wa mtu mwengine.

Uhusiano huo wa miaka miwili ulisababisha mtoto kuzaliwa na sasa Mariri ni mjamzito wa mtoto wa pili.

Mariri ameondoka katika nyumba hiyo, akiwaacha nyuma watoto sita na Ibrahim. huku Bala akiambiwa na polisi kutoondoka Kano kwa kuwa wanaendelea kuchunguza kesi hiyo.

Gwani Murtala , kamanda wa kituo cha polisi cha Kumbotso ambako tukio hilo lilitokea aliambia BBC kwamba kesi hiyo ni ya kwanza kuwahi kufanyika na kwamba hajui jinsi itakavyoisha.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,554FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles