Raymond Minja – Iringa
Wakati dunia ikiwa katika taharuki ya ugonjwa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona, uongozi wa shule za Star Intalinational Iringa, umezindua mfumo mpya wa ufundishaji wa wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi nchini kwa njia ya mitandao ya kijamii (Online) ambapo wanafunzi watafundishwa wakiwa majumbani.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua mpango huo wa ufundishaji kwa njia ya mtandao Mkurugenzi wa shule Star Intalinational Iringa, Dk. Jesca Msambatavangu amesema kuwa mfumo huo utamwezesha mwanafunzi wa sekondari na na shule za msingi kuweza kuendelea na masomo kama kawaida kwa wakati huu ambao shule zimefungwa kwa garama ndogo.
“Kutokana na changamoto ya corona ambavyo imeitikisa dunia sisi kama wadau wa elimu tumeona kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuangalia namna gani ya kuwasaidia watoto wa Tanzania ambao kwa sasa wanaendelea kukaa nyumbani pasipo kufundishwa kama apo awali.
Amesema kupitia mfumo huo wa kimtandao wameweka utaratibu wa kila darasa ndani ya wiki kuweza kukutana na mwalimu kwa njia ya mtandao ambapo wanafunzi wataweza kufundishwa moja kwa moja na kuweza kuuliza maswali mbalimbali ya kimasomo kutokanana kazi walizopewa.
Ameongeza kuwa mfumo huo wa ufundishaji utawalenga wanafunzi wote nchini wanaosoma sekondari na shule za msingi ili waweze kuendelea na masomo yao wakiwa nyumbani ambapo watatakiwa kujiunga na tovuti ya www.coronaseasonschool.com ili kuwa miogoni mwa wanafunzi watakaopata fursa ya kufundishwa.
Aida amesema anaendelea na mchakato wa kuwezesha mfumo huo kufundisha masomo nchi zote za Afrika na kuwa wameamua kuweka gharama ndogo ili wazazi waweze kumudu na kwamba hata pale shule zitakapofunguliwa mfumu huo utakuwa ni endelevu.