27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mdau wa elimu abuni mbinu ya wanafunzi kusoma kwa njia ya mtandao

Raymond Minja – Iringa

Wakati dunia ikiwa katika taharuki ya ugonjwa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona, uongozi wa shule za Star  Intalinational Iringa, umezindua mfumo   mpya  wa ufundishaji  wa  wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi nchini kwa  njia ya mitandao ya  kijamii (Online)  ambapo  wanafunzi  watafundishwa   wakiwa  majumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua mpango  huo wa  ufundishaji  kwa  njia ya mtandao  Mkurugenzi wa  shule Star  Intalinational Iringa, Dk.  Jesca  Msambatavangu amesema  kuwa  mfumo  huo utamwezesha  mwanafunzi wa  sekondari na na  shule za msingi  kuweza  kuendelea na masomo kama  kawaida  kwa  wakati huu ambao  shule  zimefungwa  kwa garama ndogo.

“Kutokana na changamoto ya  corona ambavyo  imeitikisa  dunia   sisi kama   wadau wa  elimu  tumeona  kila mmoja kwa nafasi yake  anapaswa  kuangalia  namna gani ya  kuwasaidia   watoto  wa Tanzania  ambao kwa sasa  wanaendelea  kukaa nyumbani pasipo  kufundishwa kama apo awali.

Amesema kupitia  mfumo  huo  wa  kimtandao  wameweka utaratibu wa  kila darasa   ndani ya wiki  kuweza  kukutana na mwalimu  kwa  njia ya mtandao ambapo  wanafunzi  wataweza  kufundishwa moja  kwa moja na  kuweza  kuuliza maswali  mbalimbali  ya kimasomo  kutokanana  kazi  walizopewa.

Ameongeza kuwa mfumo  huo wa ufundishaji  utawalenga  wanafunzi   wote  nchini wanaosoma  sekondari na  shule za msingi  ili  waweze kuendelea na masomo  yao wakiwa nyumbani ambapo watatakiwa   kujiunga na tovuti ya  www.coronaseasonschool.com ili kuwa miogoni mwa wanafunzi watakaopata fursa ya kufundishwa.

Aida amesema anaendelea na mchakato  wa kuwezesha mfumo   huo  kufundisha masomo  nchi  zote za Afrika  na  kuwa  wameamua  kuweka gharama ndogo  ili wazazi waweze kumudu na kwamba hata pale shule  zitakapofunguliwa mfumu  huo utakuwa ni endelevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles