Habari wakuu, ujumbe wangu kwa bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu (HESBL). Kuna watu hawana uwezo hawakupata mkopo, kisha kuna watu wanauwezo wa kulipa wanapewa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu.
Kuna wengine hawahitaji hata kufanyiwa vetting (Uhakiki) wanajulikana pesa wanazo kwa nini wasilipe wenyewe ili hizi nafasi za mikopo wapewe wanafunzi wasio na uwezo wa kulipa?
Naomba HESBL watowe priority (kipaumbele) kwa wanafunzi wasio na uwezo. Kuna watu wanajulikana uwezo wa kulipa wanao na wengine ambao hawajulikani wafanyiwe vetting (uhakiki) ili hii mikopo iende kwa wanafunzi waliolengwa wasio na uwezo.
Je. tumewahi kufanya utafiti wanafunzi wangapi wanaacha kusoma baada ya kukosa mkopo?
Mfano, mwaka jana kiongozi wa juu wa Serikali anapata mkopo, nafasi hiyo ilikuwa iwe msaada kwa mwanafunzi asiyeweza kujilipia.
Labda kama kuna sehemu nimekosea, naombwa kurekebishwa. Lakini uwazi na haki inahitajika zaidi wakati wa utoaji wa mikopo ya elimu ya juu.
Walau upande wetu tusipoteze wasomi wanaotaka kusoma, Taifa linataka wasomi zaidi.
Mahesh Shah-Mdau wa Elimu nchini.