27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

MCT yawapiga msasa wanahabari Kilimanjaro

Na Amina Omari, Moshi

Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na shirika la Pathfinder wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kuripoti masuala ya idadi ya watu katika kujiletea maendeleo.

Akifungua mafunzo hayo leo Desemba 17, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Kilimanjaro, Meck Mustafa amesema mafunzo hayo yatasaidia waandishi kuweza kuhabarisha umma kwa weledi na ufanisi zaidi.

“Siku zote kalamu zetu zimekuwa zikiripoti mazuri na mabaya yaliyoko katika jamii, hivyo tumieni mafunzo haya kuelimishs hii dhana ya idadi ya watu ili wananchi waweze kuielewa na kuweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi,” amesema Mstafa.

Kwa upande wake Afisa programu wa MCT, Paul Malimbo amesema kuwa wametayarisha mwongozo ambao utasaidia waandishi wa habari kuripoti kwa wekedi dhana hiyo.

Nae, Mwakilishi wa shirika la Pathfinder Meshack Mollel amesema iwapo nchi yetu itatumia idadi ya watu vizuri kwa miaka 40 ijayo itaweza kufikia malengo makubwa ya kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles