DC Butiama aipongeza CRDB kuwezesha wanawake

0
345

Na Shomar Binda, Butiama

Mkuu wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Anna Nyamubi ameipongeza benki ya CRDB kwa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali na kuwapa mikopo isiyokuwa na riba kubwa.

Akizungumza leo Alhamis Desemba 17, kwenye warsha ya wanawake iliyoandaliwa na benki hiyo mjini Musoma,amesema wanawake wanaopitia kwenye benki hiyo wengi wamefanikiwa na wanaokwama wamekuwa wakiinuliwa.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anna Nyamubi akizungumza na wanawake katika warsha iliyoandaliwa na benki ya CRDB

Amesema benki ya CRDB imekuwa mdau mkubwa wa serikali katika kushirikiana na kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanawake na kupitia warsha waliyoileta mkoa wa Mara itawakomboa wengi.

“Nipongeza benki ya CRDB kwanza kwa elimu ya ujasiliamali kwa wanawake na kutoa mikopo isiyokuwa na riba kubwa na tuitumie fursa hii vizuri kusikiliza mada zitakazotolewa,”amesema Nyamubi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here