25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji Mallasy anusulika kwenda jela

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imekubali maombi ya mdai Prosper Rweyendera kubadilisha maombi yake ya kutaka kumpeleka jela mdaiwa Mchungaji Godfrey Mallasy kwa kushindwa kulipa Sh milioni 139 badala yake wawasilishe maombi ya kukamata mali.

Mahakama imefikia hatua hiyo jana baada ya mdaiwa Mallasy kushindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kuomba alipe Sh milioni 12 huku mdai akitaka kiasi hicho kilipwe kama ilivyoamriwa na mahakama.

Mchungaji Mallasy alidai kwamba alikutana na wakili wa mdai Evodius Rutabingwa kueleza mpango wake wa kulipa deni hilo.

Alidai kwamba kesi ilikuwa ya Kanisa la City Christian Fellowship lililokuwa Sinza Palestina Dar es Salaam, na yeye alikuwa kiongozi lakini baada ya mgogoro huo kumalizika, kanisa lilisambaratika na kubaki yeye peke yake.

“Niliomba mdai anisamehe na alipokataa niliomba nilipe Sh milioni 12 ambapo kila mwezi nilipe Sh 200,000 kwa sababu sina kipato kwani nilikuwa nategemea kanisa ambalo kwa sasa halina waumini.

“Hivi sasa napata fedha pale napoitwa kwenda kutoa mada,”alisema.

Wakili wa Mdai Rutabingwa alidai ni kweli mdaiwa aliomba kupunguziwa fedha hizo kutoka Sh milioni 139 hadi Sh milioni 12.

Alidai kwa mazingira ya kesi mteja wake alikataa na kuomba alipwe kiasi hicho kama ilivyoamriwa na mahakama na akishindwa wanaomba amri ya kumpeleka gerezani.

“Nawashauri mfanye marekebisho ya maombi yenu ya kumpeleka gerezani kwani magereza yetu kwa wahalifu wetu hayatoshi hata kama mteja ana uwezo wa kulipa gharama za kuishi huko kama kuna mali mfanye marekebisho na ombi la kwanza liwe kukamata mali.

“Suala la kwenda gerezani hufanyika endapo mdaiwa hana mali,, “alisema Naibu Msajili Safina Semfukwe.

Baada ya kueleza hayo, Naibu Msajili Semfukwe alimtaka mdaiwa kuangalia anafanyaje ili kulipa hilo deni kwani kesi ipo kwa jina lake

“Wakati hawa wanaendelea kuwasilisha maombi, wewe uangalie namna ya kulipa deni kabla amri ya kukamata nyumba haijatolewa,” alisema Naibu Msajili na kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12,2021.

Aprili 2016 Mahakama hiyo iliamuru kanisa hilo liondolewe mara moja na kumuachia mdai eneo lake.

Uamuzi ulitolewa na Jaji John Mgeta na hukumu kusomwa na Msajili Richard Kabate. Aliamuriwa kulipa kodi ya Sh milioni moja kila mwezi tangu walipoacha kulipa kodi hiyo mwaka 2004.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles