27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mchugaji awataka waumini wake kutii mamlaka

DERICK MILTON – BARIADI

MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Bariadi, Greyson Kinyaha, amewataka waumini wa kanisa hilo kutii na kuziheshimu mamlaka zilizowekwa na Mungu kwenye Serikali na dini.

Alisema kuwa mamlaka zilizopo hazikujiweka zenyewe, bali zimewekwa na Mwenyezi Mungu na hakuna budi kwa kila muumini na Mkristo kuhakikisha anazitii.

Hayo aliyasema juzi wakati akiongoza ibada ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa la Usharika wa Tumaini mjini hapa.

Alisema kuwa mamlaka hizo zimetajwa na Mungu hivyo ni halali.

Akitumia Biblia Waraka wa Kwanza wa Petro, sura ya tano, mstari wa sita alisema; “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari ili awakweze kwa wakati wake.”

Aliwataka waumini kutafakari kwa kina maneno ya mstari huo.

“Siyo kwamba mamlaka mbalimbali ikiwemo Serikali au dini zimejileta, hapana, zimetoka kwa Mungu. Ni lazima kila Mkristo aweze kuzitii na kuziheshimu, tumeagizwa hivyo hata kwenye kitabu kitakatifu Biblia,” alisema Mchugaji Kinyaha.

Aliwataka waumini hao kuheshimiana na kutojikweza kwa kuonyeshana mabavu kwani hapa duniani haviwezi kusaidia na wataulizwa mbinguni siku wakifika.

“Kuna watu wengine wanajiona wana nguvu za kipesa hata kazi, wanajiona wao wana uwezo mkubwa kuliko wengine, lazima watu tuheshimiane maana hatujui siku wala saa, mkubwa amheshimu mdogo na mdogo vivyo hivyo,” alisem.a

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles