26.2 C
Dar es Salaam
Friday, December 3, 2021

‘Jamii isiwatenge waathirika dawa za kulevya’

Amina Omari – Tanga

JAMII imeaswa kuwaonesha upendo na kuwajali waathirika wa dawa za kulevya ili waweze kupata nafuu ya haraka badala ya kuwatenga kama ilivyo sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji wa Kanisa la Gloryland, Manase Maganga, wakati akikabidhi msaada kwa vituo vya kulea waathirika wa dawa za kulevya jijini hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi.

“Sisi kama kanisa tumeamua kuwapa msaada ili watu hao wajione ni sehemu ya jamii na kwamba wajione kama matukio waliyoyapata ni bahati mbaya na wataweza kujirekebisha na kurudi katika hali yao ya awali,” alisema Mchungaji Manase.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Gift of Hope, Said Bandawe, aliiomba Serikali kuharakisha tiba ya methadone ili kuweza kuwanusuru waathirika wa dawa za kulevya.

Alisema kuwa tiba hiyo itaweza kuwa unafuu wa haraka kwa watumiaji wa madawa lakini hata uhalifu unaweza kupungua kwa kiwango kikubwa mitaani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,848FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles