29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mchezea nyoka aiomba serikali ijali sanaa za asili

NA VICTORIA PATRICK (TSJ)

MSANII anayechezea nyoka ambaye alikuwa nchini Marekani kwa takribani miaka 10, Salma Mushi, amezitaka idara zinazohusika na utoaji wa kazi za sanaa kwa watu wa nje na kwa wasanii wa ndani itende haki kwa wasanii wote nchini.

Alisema kama serikali ina uwezo wa kuwapeleka wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, kwa nini isiwape nafasi kama hiyo wasanii wa sanaa za asili kwa kuwa sanaa hizo zinatangaza nchi nje kupitia mavazi, ngoma na muziki wa asili, kiasi cha kuvutia watalii wengi kuja kutazama maliasili nchini Tanzania.

Mwanamama huyo alizungumza hayo jana, alipokuwa katika jukwaa la sanaa linaloendeshwa katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Aliongeza kwamba, sanaa za asili kwa Tanzania zinaelekea kufa kama hazitapewa kipaumbele kinachotolewa kwa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles