Mc Pilipili anogesha mahafali Mwl. Nyerere

0
1019
Emanuel Mathias ‘Mc Pilipili’
Emanuel Mathias ‘Mc Pilipili’
Emanuel Mathias ‘Mc Pilipili’

NA SALMA MPELI –DAR ES SALAAM

MSANII wa vichekesho nchini, Emanuel Mathias ‘Mc Pilipili’, amekonga nyoyo za watu katika mahafali ya 18 ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Mwalimu Julias K. Nyerere iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.

Mbali na Mc Pilipili, katika mahafali hayo yaliyopambwa na michezo na burudani mbalimbali, wanafunzi wenye vipaji vyao ikiwemo kucheza muziki na ngoma za asili kwa uwezo wa hali ya juu wakiwashangaza wazazi na walezi wao waliohudhuria mahafali hayo.

Mwalimu wa michezo shuleni hapo, Beno Mbilo, alisema kazi ya kuwafundisha wanafunzi michezo na sanaa mbalimbali walizoonyesha imetokana na ushirikiano wa shule hiyo na wasanii kutoka Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo.

“Tumeshirikiana na wasanii kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo, lakini pia imekuwa rahisi kwetu kwa kuwa wanafunzi wanapenda sanaa waliyoifanya mbele ya wazazi na walezi wao,” alieleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here