29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge wa Nkasi ahofia kuonekana mzembe

Godfrey-ZambiMBUNGE wa Nkasi Kusini, Desdurius Mipata (CCM), amehofia wapiga kura wake kumuona mzembe kutokana na kushindwa kupeleka huduma ya mawasiliano katika jimbo lake.

Akiuliza swali bungeni jana, alisema licha ya kuihoji Serikali mara kwa mara, lakini hadi sasa vijiji hivyo havina mawasiliano.

“Je, Serikali haoni wananchi wangu wataniona mzembe kwa kushindwa kuwapelekea mawasiliano,” alihoji.

Alitaka kujua mpango wa Serikali wa kuvipatia vijiji vya kata ya Kate na Isale mawasiliano ya uhakika.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Godfrey Zambi, aliwahakikishia wananchi wa Nkasi Kusini kuwa mbunge wao si mzembe.

“Mbunge wao anafanya kazi vizuri, kampuni za simu zinafanya kazi kwa awamu, hivyo itayafikia maeneo yote hayo hatua kwa hatua.

“Kata za Kate na Isale katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa zimejumuishwa katika mawasiliano vijijini awamu ya pili unaosimamiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF).

Alisema kampuni ya Tigo imeshinda zabuni na mradi huo unatarajiwa kukamilika Januari 21, mwakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles