Na Mwandishi Wetu, Sengerema
Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Hamis Tabasamu amemwagiza Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Clement Kihinga, kufanyia kazi changamoto alizozibaini katika utengenezaji wa barabara yenye urefu kwa kilometa Nne kutoka kata ya Ibondo kuelekea stendi mpya ya Sengerema.
Tabasamu ametoa maelekezo hayo wakati alipofanya ukaguzi juzi katika barabara hiyo inayotengenezwa kwa gharaa ya Sh milioni 140.
Aidha , amefafanua kuwa hatakubali kupokea mradi huo iwapo utakuwa chini ya kiwango ambapo ameishauri ofisi ya Tarura ambao ni wasimamizi kuhakikisha barabara hiyo inatengenezwa kwa kiwango kutokana na kuwa na matumizi makubwa ya kupitisha magari mengi yaendayo mikoani.
Mkadarasi wa kampuni TEKI ambaye anatengeneza barabara hiyo, Boas Kamara, amesema matengezo yamefika aslimia 98 na itakabidhiwa Mwezi huu badala ya Julai 7, 2021 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Tarura, Samu Majengo alithibitisha kuwa barabara hiyo itagharimu Sh milioni 146 na Mkadarasi hajalipwa fedha zote huku akisema ofisi yake imepokea ushauri wa mbunge na itaufanyia kazi kabla ya kukabidhiwa barabara hiyo.