23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wanachama SADC watakiwa kutengeneza chanjo

Na Mwandishi Wetu

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), imetakiwa kuimarisha uwezo wa ndani wa kutengeneza chanjo na dawa ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa dawa na chanjo panapotokea majanga na magonjwa ya milipuko inayosababisha vifo vingi katika Bara la Afrika.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji SADC,Dk. Stergomena Tax , wakati akitoa taarifa ya utendaji ya Jumuiya hiyo katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC na kuongeza kuwa janga la UVIKO -19 limekuwa na changamoto kubwa husasani katika upatikanaji wa chanjo kwa wananchi wote wa jumuiya hiyo.

Dk. Tax ambaye ameitumia fursa hiyo kuwaaga mawaziri wa SADC baada ya kumaliza muda wake, amezisihi nchi za Afrika kuweka nguvu za pamoja katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 na kuziomba nchi,taasisi na Jumuiya za Kimataifa kuridhia nchi masikini  kutumia teknolojia zao katika kuzalisha dawa na chanjo ili huduma hiyo ipatikane kwa wananchi wote.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ambaye ameongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi, amezitaja baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na kumchagua mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu,amesema Tanzania imeendelea kuwa mfano katika kufuata sheria na taratibu za Jumuiya mbalimbali ambazo ni mwanachama ikiwa ni pamoja na ulipaji wa ada kwa wakati.

Mkutano huu wa siku mbili wa Baraza la Mawaziri wa SADC ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17- 18, 2021 Lilongwe nchini Malawi na Tanzania itawakilishwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na mambo mengine utaidhinisha nyaraka mbalimbali za kisheria ikiwemo itifaki ya takwimu.

.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles