27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Matiko aeleza walivyosotea viapo vya mawakala wao

Kulwa Mzee, Dar es salaam

MBUNGE wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema), amedai mahakamani kwamba anamiliki silaha (bastola) aina ya revolver lakini hajawahi kuitumia na hakumbuki kama iliwahi kuftuka mahali popote, huku akieleza walivyosotea viapo vya mawakala wao.

Mshtakiwa huyo alidai hayo jana wakati akijitetea mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Matiko ni mshtakiwa wa tano ambaye jana alikuwa akiongozwa kujitetea na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala.

Alidai pamoja na  kumiliki silaha hiyo hajawahi kuitumia wala hakumbuki kama iliwahi hata kufyatuka mahali popote.

Akizungumzia kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni, alidai baada ya kufika Dar es Salaam alikabidhiwa jukumu la kufuatilia nakala za viapo na barua za utambulisho wa mawakala.

“Nilitoka Tarime Mjini Februari 15, nilipofika Dar es Salaam niliwasiliana na mmoja wa viongozi wa Kamati ndogo ya uchaguzi Benson Kigaila kwa simu kumfahamisha kuwa nimefika, alinipa jukumu la kufuatilia barua za utambulisho pamoja na hati za viapo vya mawakala.

“Jukumu nilipewa mimi na Mbunge Suzan Lyimo, tulianza kufuatilia barua hizo Februari 16, mwaka 2018 saa nne asubuhi , tulikwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ambaye ndiye alikuwa Msimamizi wa Uchaguzi huo ili aweze kutusaidia kupata barua huzo.

“Tukipofika ofisini kwa Mkurugenzi tuliambiwa tusubiri mpaka tulipoonana naye saa saba mchana lakini alituambia anashughulikia jambo hilo hivyo tusubiri mpaka saa 12,”alidai.

Alidai walisubiri mpaka saa 12 lakini hawakufanikiwa kupata barua hizo na mkurugenzi aliwahakikishia watapata hizo barua mpaka kufikia saa moja usiku wa siku hiyo.

Matiko anadai walichukua mawasiliano ya Msimamizi wa Uchaguzi na msaidizi wake na waliendelea kuwasiliana na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi aliyemtaja kwa jina la Victoria Charles mpaka saa tano usiku.

Anadai msimamizo huyo alionekana kutingwa na kazi ya kusambaza vifaa vya uchaguzi hivyo akashindwa kumpatia barua hizo na kumuahidi kuwa atawasiliana naye saa 11 alfajiri ya Februari 17, mwaka 2018 ambayo ndiyo ilikua siku ya uchaguzi.

Alidai mpaka kufikia saa 11 alfajiri barua na nakala za viapo hivyo zilikuwa hazijapatikana, alitoa taarifa kwa Msimamizi wa Uchaguzi na baadaye kwa viongozi wa Kamati Ndogo ya Uchaguzi na jukumu lake likaishia hapo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,  Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Kibamba John Mnyika na  Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini,  Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles