Watoto 48 wafanyiwa upasuaji wa moyo JKCI

0
900

Aveline Kitomary, Dar es salaam

JUMLA  ya Watoto 48 wenye magonjwa ya moyo  wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa kufungua kifua na upasuaji wa tundu dogo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI).

Matibabu hayo ya Moyo kwa watoto yamefanywa na madaktari bingwa kutoka Saudi Arabia wanashirikiana na madaktari wa JKCI katika kambi ya siku ya siku saba inayofanyika katika Taasisi hiyo ambayo pia yamehusishwa upimimaji wa watoto.

Akizungumzia na MTANZANIA  jana jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji Angela Muhozya alisema  kwa asilimia kubwa ya watoto waliofanyiwa upasuaji ni wale waliozaliwa na matatizo ya Moyo kama matundu na matatizo ya mishipa.

“Tumeanza upasuaji kuanzia Jumapili siku hiyo tumefanya upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto watano, Jumatatu tulifanya kwa watoto watano,jumanne watoti wanne na jana jumatano watoto walikuwa sita.

“Katika upasuaji wa bila kufungua kifua tulianza jumatatu ambapo watoto saba walipata huduma siku ya jumanne watoto nane na leo Jumatano tunaowafanyia watoto 12,”alibainisha.

Kwa upande wake mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake alifanyiwa upasuaji Rose Msaki alisema mtoti wake Juniour Mollel alikuwa na tatizo la kuwa tundu moja ambayo ilikuwa imepitisha damu safi na chafu.

“Aliugua kwa muda wa mwaka na mwezi mmoja tulijua anatatizo la nimonia akiwa na miezi miwili kuna daktari akaniambia nimlete hapa afanyiwe uchunguzi wa moyo sasa wamefanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri naishukuru serikali yetu na ya Saudi Arabia,”alieleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here