27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Lugangira atoa elimu ya Uviko-19

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 
 
MBUNGE wa Viti Maalumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewakilisha Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs), Neema Lugangira ametoa elimu ya Uviko-19 kwa Wenyeviti na Makatibu wa matawi yote ya UWT, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
 
Lengo la elimu hiyo ni kuwaongezea hamasa na uelewa sahihi juu ya ugonjwa huo na umuhimu wa chanjo yake inayoendelea kutolewa.

Akizungumza jana wakati akitoa mafunzo hayo yaliyofanyika Kijiji cha Kizimkazi, Makunduchi alipozaliwa Rais Samia Suluhu Hassan, elimu iliyoenda sambamba na iliyoenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya UWT, alisema wameamua kutoa elimu hiyo kwa viongozi hao ili iweze kufika katika ngazi ya jamii kwa urahisi.
 
Mbunge huyo ambaye pia ni Balozi wa Kitaifa wa Uviko-19 alisema anatarajia kufikisha elimu hiyo kwa makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini na wanahabari katika mikoa iliyopo hatarini zaidi na kuwa atashirikiana na wadau wengine katika kufanikisha kampeni hiyo.
 
Alisema wameanza kutoa elimu kwa kundi hilo ambapo wanaamini wao kama viongozi wa kisiasa wamekuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii hivyo watasaidia kupunguza upotoshwaji katika jamii hivyo jamii inahitaji elimu sahihi itakayowawezesha kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo.
 
“Tumeamua kutoa elimu hiyo ili kuweza muweze kupata uelewa namna ya kujikinga na Uviko -19 kwa kuhakikisha mnatumia hiari yenu na kupata chanjo ya ugonjwa,mtakapopata elimu hii tunaamini mtaenda kuelimisha jamii na kuwahamasisha juu ya akujilinda na kupata chanjo,” amesema. 
 
Alisema ni muhimu jamii kuwa  na uelewa wa ugonjwa huo ikiwemo suala la usalama wa chanjo na kuwawezesha kuweza kutumia hiari yao vizuri kuweza kuchagua chanjo ya uviko 19 ambayo ni salama na inawapunguzia madhara ikiwemo kifo pale wanapopata ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles